ARSENAL
wako kwenye wasiwasi mkubwa wakisubiri kujua hali ya Fowadi wao Alexis
Sanchez ambae ameumia Musuli za Mguuni akiwa Mazoezini na Timu ya Taifa
ya Nchi yake Chile.
Chama cha Soka cha Chile kimetoa Taarifa kuthibitisha kuumia kwa
Sanchez na kusema Mchezaji huyo atabaki Santiago, Chile wakati Timu
inasafiri kwenda kucheza na Colombia Alhamisi Usiku kwenye Mechi ya
Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini kuwania kufuzu kucheza Fainali za
Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Kisha Chile itarejea kwao kucheza na Uruguay hapo Jumanne Novemba 15.
Sanchez, mwenye Miaka 27, Msimu huu ameifungia Arsenal Bao 8 na ikiwa atakaa nje kwa muda mrefu ni pigo kubwa kwa Timu yake.
Mechi inayofuata kwa Arsenal baada ya Wiki hizi 2 za Mechi za
Kimataifa ni dhidi ya Manchester United huko Old Trafford hapo Jumamosi
Novemba 19 ikiwa ni Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, na kisha ni ile ya
UEFA CHAMPIONZ LIGI Jumatano Novemba 23 dhidi ya Paris Saint-Germain
Mechi ambayo ni muhimu kuamua nani ataibuka Mshindi Kundi A.
No comments:
Post a Comment