Na Ally Daud-MAELEZO.
MAMLAKA
ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikia kukusanya shilingi trilioni 1.15
kwa mwezi Oktoba ikiwa ni kukamilisha malengo waliyojiwekea katika
ukusanyaji wa mapato.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi Bw. Richard
Kayombo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam kuhusu hali ya makusanyo na zoezi la uhakiki wa namba za
utambulisho wa mlipa kodi (TIN)linaloendelea hivi sasa.
“Tumefanikiwa
kukusanya shilingi Trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa ni
kufanikisha malengo ya ukusanyaji kodi nchini ili kukuza uchumi wa nchi
pamoja kusaidia Serikali kuendeleza huduma za jamii nchini” alisema Bw. Kayombo.
Aidha
Bw. Kayombo amesema kuwa mapato hayo yametokana na mikakati thabiti
iliyowekwa na mamlaka hiyo katika ukusanyaji kodi hapa nchini ili kuweza
kusaidia ongezeko la pato la Taifa .
Katika
hatua nyingine TRA imefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 zilizokuwa
zikiendelea katika mahakama mbalimbali nchini dhidi ya walipa kodi wake
na kufanikiwa kupata kiasi cha takribani Bilioni 16.9 .
“Tumefanikiwa
kushinda kesi 9 kati ya 10 ambazo zilifikishwa mahakamani dhidi ya
walipa kodi na kupata kiasi cha shilingi bilioni 16.9 hivyo kufanya
juhudi zetu za kukusanya mapato mengi zaidi” aliongeza Bw. Kayombo.
Mbali
na hayo Bw. Kayombo amesema kuwa zoezi la uhakiki wa namba za
utambulisho wa mlipa kodi ambalo limeanza hivi karibuni linaendelea na
litafikia tamati Novemba 30 mwaka huu kwa mkoa Dar es salaam hivyo
wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya uhakiki huo.
Aidha
Bw. Kayombo ameongeza kuwa kila mwenye namba ya utambulisho wa mlipa
kodi anatakiwa akahakiki kwa ajili ya kupata taarifa sahihi za mlipa
kodi ili kuepuka kufutwa kwa namba yake ya utambulisho baada ya zoezi
hilo kumalizika kwa mkoa husika.
No comments:
Post a Comment