TRENI ya abiria inayofanya safari zake kati ya Kituo Kikuu cha Reli na maeneo ya Pugu Dar es Salaam maarufu kama ‘Treni ya Mwakyembe’ nusura ichomwe moto juzi, baada ya wananchi kudai kuchoshwa na usumbufu wa shirika hilo.
Wananchi
hao walitaka warudishiwe nauli zao kwa kile walichodai Shirika la
Reli Tanzania (TRL) limeshindwa kuwa na ratiba inayoeleweka.
Tukio
hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la Majumbasita, baada ya treni
hiyo kukaa kituoni hapo kwa muda mrefu bila kuambiwa kuambiwa chochote.
Hali
hiyo iliwafanya abiria kuvamia kituo kidogo cha mawasiliano kilichopo
eneo hilo wakitaka warejeshewe nauli zao vinginevyo wangekichoma moto
pamoja na mabehewa ya treni hiyo.
Mwandishi
aliwashuhudia abiria wakitaka kuingia ndani ya kituo hicho huku
wakiwalazimisha wafanyakazi waliokuwapo wawarudishie fedha zao za nauli.
Purukushani hiyo iliyodumu kwa takribani saa mbili ilimalizika kwa abiria hao kuvunja vioo vya mabahewa ya treni vipatavyo 30.
Wafanyakazi
kuona hivyo walijifungia ndani ya kituo hicho huku polisi waliokuwa
wakisindikiza treni hiyo wakitimua mbio kunusuru maisha yao.
Baadhi
ya abiria walisema tangu Ijumaa iliyopita wamekuwa wakipata
usumbufu kwa kukatishiwa tiketi huku treni ikichelewa na wakati
mwingine kutoonekana kabisa.
Walisema
jambo hilo limekuwa likiwasababishia hasara na kuwalazimu kutafuta
usafiri mwingine na kuchelewa kufika kwenye majukumu yao.
“Tukio hili si mara ya kwanza kujitokeza, lilijitokeza tarehe 24, 26 na 28 mwezi wa 10 na Novemba 7 Katika matukio hayo kulitokea uharibifu wa miundombonu na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi wa TRL akiwemo Mustapha Omary ambaye ameshonwa nyuzi 8 katika hospitali ya mnazi mmoja,” amesema.
Amesema kutokana na uharibifu huo, watuhumiwa 17 wanashikiliwa na jeshi la polisi na kwamba upepelezi ukikamilika watachukuliwa hatua za kisheria.
Kadogosa amedai kuwa, wahusika wa fujo na uharibifu huo ni makondakta wa dalala kwa lengo la kutisha wananchi kutoutumia usafiri wa treni.
“Kuna watu wa daladala wanafikiri wataendelea kufanya fujo ili wananchi waone kuwa usafiri wa treni si salama wapande magari yao, sisi hatulazimishi wananchi kuutumia usafiri wetu ila kutokana na ubora wa huduma zetu wanakuja wenyewe. Pia hatusitishi kutoa huduma kwa sababu ya fujo zao sababu tutawatesa abiria wetu zaidi ya 21,000,”
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Reli, Simon Chillery amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini wengine waliohusika.
No comments:
Post a Comment