Waziri
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amepokonywa na Serikali shamba lake
lenye ukubwa wa hekta 33 kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuliendeleza.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa Serikali imefikia uamuzi
huo baada ya Sumaye kushindwa kuliendeleza kama notisi ya siku 90
ilivyoeleza.
“Oktoba
28, mwaka huu. Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi
ya shamba namba 3074 lililopo Mabwepande. Shamba hili lilikuwa na hati
namba 53086. Jina la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline
Sumaye,” amesema Hapi.
Sumaye
ambaye alikuwa ni mmoja wa wasemaji tegemeo katika mikutano ya kampeni
ya Uchaguzi Mkuu uliopita ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
anamiliki mashamba makubwa yaliyoko Morogoro na Mabwepande Dar es
Salaam.
Baada ya Rais Magufuli kubatilisha hati hiyo, Hapi amesema kuanzia sasa ni marufuku kwa Sumaye kujihusisha na shamba hilo.
Kwa sababu hati yake imeshabatilishwa na akibainika kufanya chochote vyombo vya dola vitachukua nafasi yake.
“Vyombo
vya ulinzi na usalama watakuwapo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba shamba
hili halitafanyiwa shughuli zozote, isipokuwa baada ya taratibu za
manispaa zitakapofanyika,” amesisitiza Hapi.
Amesema
amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Aron
Kagurumjuli kupima viwanja vya shamba hilo na kwamba wananchi waliokuwa
na mgogoro wa shamba hilo wafikiriwe.
Februari
5 mwaka huu, akiwa Morogoro, Rais John Magufuli aliwataka watu wote
waliotelekeza mashamba kuyaendeleza, la sivyo atawanyang’anya na kuwapa
wananchi.
No comments:
Post a Comment