UEFA CHAMPIONZ LIGI: BARCA, CITY ZASONGA, ARSENAL HALI TETE KUKOSA USHINDI WA KUNDI! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 24, 2016

UEFA CHAMPIONZ LIGI: BARCA, CITY ZASONGA, ARSENAL HALI TETE KUKOSA USHINDI WA KUNDI!


>>TIMU 12 ZAFUZU BADO 4!
UEFA CHAMPIONZ LIGI</strong>
Matokeo Mechi za 5 za Makundi
Jumatano 23 Novemba 2016
KUNDI A
Arsenal 2 Paris Saint Germain 2            
Ludogorets Razgrad 0 FC Basel 0          
KUNDI B
Besiktas 3 Benfica 3         
Napoli 0 Dynamo Kiev 0             
KUNDI C
Borussia Monchengladbach 1 Manchester City 1
Celtic 0 Barcelona 2
KUNDI D
FC Rostov 3 Bayern Munich 2               
Atlético Madrid 2 PSV Eindhoven 0                  

Mechi za 5 za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, zimemalizika Jana Usiku na Timu 2 zaidi, FC Barcelona na Manchester City, kufuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 hapo Jana huku wakibakisha Mechi 1 mkononi.
Kwenye Kundi A, Arsenal na Paris St-Germain, ambazo zilikuwa tayari zimeshafuzu, zilipambana huko Emirates Jijini London na hasa kugombea nani atakuwa Mshindi wa Kundi lakini zikatoka Sare ya 2-2 na hivyo kumkosa Mshindi wa Kundi hapo Jana ingawa sasa PSG ndio wenye nafasi kubwa ya kutwaa ushindi huo wa Kundi.
Baada ya Timu hizo kutoka 1-1 huko Paris, Jana Sare ya 2-2 imeipa PSG Bao nyingi za Ugenini na hivyo wana nafasi kubwa kutwaa ushindi wa Kundi wakipata matokeo mazuri kwenye Mechi yao ya mwisho watakayocheza huko kwao na Ludogorets Razgrad, iliyopigwa 6-0 na Arsenal, hapo Desemba 6.
Hapo Jana, PSG walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 18 la Edinson Cavani na Arsenal kujibu kwa Bao 2 za Dakika za 45 na 60 za Olivier Giroud, kwa Penati, na lile la kujifunga mwenyewe Marco Verratti.UCL-NOV23-A-D
Lakini PSG wakasawazisha zikibaki Dakika 13 kupitia Lucas na Gemu kwisha 2-2.

Timu 12 ambazo zimefuzu – Bado 4:
-Arsenal, Paris St-Germain, Atletico Madrid, Bayern Munich, Borussia Dortmund, Monaco, Bayer Leverkusen, Real Madrid, Leicester City, Juventus, Barcelona, Manchester City
Timu ambazo zimetupwa nje ya Mashindano:
-Ludogorets, Basel, PSV Eindhoven, FC Rostov, Club Brugge, Dinamo Zagreb, Legia Warsaw, Tottenham, CSKA Moscow, Sporting Lisbon, Dynamo Kiev, Borussia Monchengladbach, Celtic

Kwenye Mechi za Kundi C, Borussia Monchengladbach, wakiwa kwao, walitoka 1-1 na Manchester City wakati huko Scotland, Barcelona waliichapa Celtic 2-0 kwa Bao za Lionel Messi, moja likiwa Penati, na kutwaa Ushindi wa Kundi hili.
Huko Germany, , Borussia Monchengladbach walitangulia kufunga Dakika ya 23 kupitia Raffael na City kusawazishia Dakika ya 46 kwa Bao la David Silva.
Kila Timu ilibaki Mtu 10 kufuatia Kadi Nyekundu kwa, Borussia Monchengladbach kumkosa Stindl alietolewa Dakika ya 51 na City kumpoteza Fernandinho Dakika ya 63.
Matoke ohayo yameipa Barca Ushindi wa Kundi C wakiwa Pointi 4 mbele ya City huku kila Timu ikibakiza Mechi 1.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Mechi za 5 za Makundi
Jumanne 22 Novemba 2016
KUNDI E
CSKA Moscow 1 Bayer 04 Leverkusen 1           
Monaco 2 Tottenham Hotspur 1
KUNDI F
Borussia Dortmund 8 Legia Warsaw 4             
Sporting Lisbon 1 Real Madrid 2            
KUNDI G
FC Copenhagen 0 FC Porto 0                
Leicester City 2 Club Brugge 1
KUNDI H
Dinamo Zagreb 0 Lyon 1            
Sevilla 1 Juventus 3         
Ratiba Mechi za 6 na za mwisho za Makundi
***Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
Jumanne 6 Desemba 2016
UCL-NOV22-E-FKUNDI A
FC Basel v Arsenal
Paris Saint Germain v Ludogorets Razgrad                
KUNDI B
Benfica v Napoli               
Dynamo Kiev v Besiktas             
KUNDI C
Barcelona v Borussia Monchengladbach           
Manchester City v Celtic
KUNDI D
Bayern Munich v Atlético Madrid           
PSV Eindhoven v FC Rostov                  
Jumatano 7 Desemba 2016
KUNDI E
Bayer 04 Leverkusen v Monaco             
Tottenham Hotspur v CSKA Moscow                
KUNDI F
Legia Warsaw v Sporting Lisbon           
Real Madrid v Borussia Dortmund         
KUNDI G
Club Brugge v FC Copenhagen              
FC Porto v Leicester City
KUNDI H
Juventus v Dinamo Zagreb         
Lyon v Sevilla         

TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MAKUNDI:
Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba
Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba
Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba
Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba
Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba
Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba
MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

No comments:

Post a Comment