Korea Kaskazini yazidi kuivuruga Marekani. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 24, 2017

Korea Kaskazini yazidi kuivuruga Marekani.



Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameliamuru jeshi la nchi hiyo kuendelea kutengeneza makombora ya nyuklia yenye uwezo mkubwa zaidi wa kusafiri masafa marefu zaidi ya yale yaliyopo kwa sasa, huku Rais wa Marekani Donald Trump akisema kuwa uhusiano wao utaimarika hivi karibuni.

Rais huyo amefikia hatua hiyo mara baada ya mgogoro kati ya Marekani na Korea Kaskazini uliosababishwa na majaribio ya mara kwa mara ya silaha za nyuklia ambayo yamekuwa yakifanywa na Korea Kaskazini, kitu ambacho Marekani imekuwa ikipinga vikali.

Aidha, katika taarifa hiyo iliyotangazwa na shirika la habari linalomilikiwa na serikali la nchi hiyo KCNA, limesema kuwa agizo hilo la kutengenezwa kwa silaha hizo siyo vitisho kwa Marekani bali linafanya hivyo kwaajili ya kuongeza nguvu ya kujilinda.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni Rais wa Marekani, Donald Trump alisikika akisema kuwa anaheshimu kuona kuwa Korea Kaskazini imeanza kuiheshimu Marekani hivyo anahisi uhusiano baina yao utaendelea kuimarika.

No comments:

Post a Comment