Mtu mmoja amefariki na wawili wamejeruhiwa baada ya gari ya abiria kugonga treni eneo la Tanesco Morogoro.
Akidhibitisha tukio hilo Mganga Mkuu wa Hospitali, Frank Jacob
amesema kwamba ajali hiyo imetokea leo asubuhi, ambapo gari hilo
lililokuwa limebeba wanafunzi lilipata ajali eneo la Masika baada ya
kugonga treni na kuburuzwa umbali wa takriban mita 50 toka yalipo
makutano ya reli na barabara.
No comments:
Post a Comment