Mwanaume mmoja nchini Nigeria ambaye ameishi na mkewe kwa takribani miaka 17 bila kupata mtoto, amejiua siku chache baada ya mkewe kujifungua mapacha watatu.
Mwili wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Edward Soje (54), ulikutwa ukining’inia kwenye kamba iliyofungwa juu ya mti mkubwa katika eneola Lokoja.
Soje, ambaye ni afisa mwanadamizi wa Kogi State Teaching Service Commission (TSC), alijitoa uhai siku 10 tu baada ya mkewe kujifungua mapacha watatu wote wa kiume, katika hospitali binafsi jijini Abuja.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vyombo vya usalama, Soje alikuwa anadaiwa kodi ya nyumba ya miezi 11 hadi wakati aliojitoa uhai.
Imeelezwa kuwa alisafiri kwenda Abuja akiacha ujumbe maalum kwa mkewe ambaye ni mtumishi wa umma.Ujumbe huo ulikariri mstari wa Biblia katika kitabu cha Zaburi 121:3.
No comments:
Post a Comment