
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani
Katavi imemuhukumu Lazaro Peter Ngomalala (50) Mkazi wa Kijiji
cha Simbwesa Wilaya ya Tanganyika kifungo cha maisha jela baada
ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka tisa jina
limehifadhiwa mwanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi
Simbwesa.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa
baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa
mashitaka akiwemo mwanafunzi huyo aliyebakwa uliotplewa Mahakani .
Kabla ya kutoa hukumu hiyo Hakimu
Ntengwa alisema mtu yeyote anayefanya kitendo kama alichofanyiwa
mtoto huyo anakuwa amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha sheria
namba 130 kifungo kidogo cha kwanza na cha pili na na kifungu cha
sheria namba 131 kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu .
Alieleza kutokana na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka akiwemo mtoto
mwenyewe na mtoto mwenzake ambaye alishuhudia tukio hilo,
mahakama pasipo shaka yoyote imemwona mshtakiwa Lazaro Ngomalala
kuwa anayo hatia .
Ntengwa alisema miongoni mwa ushahidi
wa sababu zilizoifanya mahakama imtie mshtakiwa hatiani ni
ushahidi uliotolewa mahakamani na mtoto aliyebakwa na mtoto mwenzake
mwenye umri wa miaka saba licha ya kuwa na umri mdogo walitoa
ushahidi kwa ufasaha mkubwa juu ya tukio hilo.
Pia Mahakama ilijiridhisha na
ushahidi uliotolewa na muuguzi wa zahanati ya Simbesa aliyemfanyia
uchunguzi na kubaini kuwa mtoto huyo alikuwa amebakwa hali
ambayo ilimlazimu muuguzi huyo amwanzishie dawa ya kuzuia maambukizi
ya VVU.
Kabla ya kusomewa hukumu hiyo,
hakimu Ntengwa alitoa nafasi kwa mtuhumiwa Lazaro kama anayo
sababu ya msingi ya kuishawishi mahakama iweze kumpunguzia adhabu
hivyo mshitakiwa aliiomba Mahakama imwachie huru kwa kile
alichodai kuwa yeye hakutenda kos hilo bali amesingiziwa na mama
mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimdai fedha alizokuwa
anamdai baada ya kumkopesha.
Baada ya utetezi huo wa mshtakiwa
hakimu Chiganga Ntengwa alisema kutokana na mshitakiwa
kupatikana na hatia ya kifungu cha sheria namba 131 kifungu
kidogo cha cha tatu kinachoeleza mtu yoyote atakayembaka mtoto
mwenye umri wa chini ya miaka kumi adhabu yake ni kifungo cha
maisha jela.
Hivyo kutokana na mshtakiwa Lazaro
Ngomalala kupatikana na kosa hilo mahakama imemuhumu kuanzia jana
kutumkia jela kifungo cha maisha jela.
Awali kwenye kesi hiyo Wakili wa
Serikali Fravian Shiyo alidai mahakamani hapo kuwa Lazaro
alitenda kosa hilo hapo Oktoba 12 mwaka 2016 majira ya saa nne
asubuhi kijiji katika Jijiji cha Simbwesa.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio
mshitakiwa alikuta mtoto aliyemtenda kitendo hicho akiwa na
mtoto mwenzake wakiwa wanacheza jirani na nyumba yao ndipo
alipowadanganya wamfuate nyumbani kwake ili akawapatie fedha za
kununulia biscuit na soda. .
Shiyo alieleza kuwa wakati wakiwa
wanaelekea nyumbani kwa mshitakiwa walipofika kwenye eneo la
tanki la maji Lazaro alimvuta kwa nguvu mtoto huyo na kuanza
kumbaka licha ya mtoto huyo kupiga kelele lakini hakuweza kumwachia
mpaka alipo maliza haja yake .
Mwanasheria aliiambia mahakama baada
ya kufanyiwa kitendo hicho mtoto huyo aliyebakwa alikwenda
kutoa taarifa kwa wazazi wake huku akiwa analia na baada ya
kutoa taarifa kwa wazazi wake mtuhumiwa alikamatwa na askari wa
mgambo wa kijiji cha Simbwesa na kisha alifikishwa katika kituo
cha polisi.
No comments:
Post a Comment