
Mwanamke
ambaye yupo kwenye ndoa kwa miaka 55, nchini Kenya amefungua kesi
mahakamani kuomba mumewe ampe talaka kwa madai kuwa hamjali, na
anamthamini zaidi mke mdogo.
Mwalimu
huyo mstaafu, Marcella Mukami Kinyugo (73), anaiomba Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kangema, isitishe ndoa yake na Peter Kinyugo (76) iliyofungwa
Septemba 16, 1962 katika Kanisa Katoliki Kiriaini.
Bibi
huyo mkazi wa mjini Kiria-ini, Mathioya, kwenye kaunti ya Murang’a, pia
aliomba apewe nusu ya mali za familia yao na pia mumewe alazimishwe
kulipa gharama za kesi.
Katika kesi hiyo bibi huyo aliwakilishwa na Margret Nyangati kutoka kampuni ya mawakili ya Muchoki Kang’ata.
Aliieleza
Mahakama kuwa, waliishi maisha ya furaha ya mume na mke tangu
walipofunga ndoa, lakini miaka sita iliyopita hali ilibadilika wakati
mumewe alipoacha kutimiza majukumu yake kama mume.
Mume
wa bibi huyo ni mwalimu mstaafu na Chifu. Mukami alidai mahakamani kuwa
matatizo yalianza baada ya Kinyugo kukaa kwa mke mdogo kwa wiki kadhaa
bila kwenda kwake, na kwamba, yeye na mke mwenzake wanaishi kwenye eneo
moja. Kwa mujibu wa bibi huyo, wakati mumewe anafanya hivyo, hawakuwa na
ugomvi.
No comments:
Post a Comment