
Mlinzi wa Simba, Jjuuko Murshid toka Ligi Kuu ya Tanzania Bara amejumuishwa ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Uganda kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji.
Mlinzi huyo licha ya kukosa namba ya kudumu kwenye kikosi cha Simba chini ya Joseph Omog na msaidizi wake, Masudi Djuma amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 26 cha Uganda.
Jjuuko aliitwa pia aliitwa kwenye kikosi cha Uganda kilichoivaa Congo Brazzaville huku hiyo ikiwa si mara ya kwanza kuaminiwa kuiongoza ngome ya ulinzi ya timu hio kwenye michezo mbali mbali.
Kikosi kilichoitwa ni:
Walinda Mlango: Isma Watenga (Vipers SC), Benjamin Ochan (KCCA FC), Nichoals Sebwato (Onduparaka FC) Ikara Tom (Kirinya Jinja SS)
Wachezaji wa ndani: Wadada Nicholas (Vipers SC), Kiyemba Ibrahim (Sc Villa Jogoo), Isaac Muleme (KCCA FC), Aggrey Madoi (Police FC), Juuko Murushid (Simba-Tanzania), Timothy Awanyi (KCCA FC), Savio Kabugo (Proline FC), Bernard Muwanga (Sc Villa Jogoo), Tom Masiko (Vipers SC), Mutyaba Muzamiru (KCCA FC), Tadeo Lwanga (Vipers SC), Stephen Mugisha (Police FC).
Wengine ni Karisa Milton (Vipers SC), Mucureezi Paul (KCCA FC), Allan Kateregga (KCCA FC), Allan Kyambadde (Sc Villa Jogoo), Nelson Senkatuka (Bright Stars FC), Derick Nsibambi (KCCA FC), Hood Kaweesa (Police FC), Batte Seif (Bright Stars FC), Saddam Juma (KCCA FC), Daniel Isiagi (Proline FC), Basse Methodious (Mbarara City FC).
No comments:
Post a Comment