Kwa Ufupi (Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma)
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge amemtembelea na
kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma
Balozi Mstaafu Job Lusinde ambapo mwenyekiti huyo wa Wazee
amemuhakikishia Dkt. Mahenge ushirikiano kutoka kwa Wazee wakati wote wa
uongozi wake Mkoani Dodoma.
Dkt.
Mahenge alimtembelea Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Balozi (Mstaafu)
Lusinde kwa lengo la kujitambulisha kama Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma na
kuahidi kuwa atakutana na Baraza zima la Wazee la Mkoa wa Dodoma hivi
karibuni, aidha, Dkt. Mahenge alipata pia fursa ya kumtembelea Waziri
Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya
Mji wa Dodoma na kujionea shughuli za kilimo na ufugaji wa kisasa wa
mifugo, nyuki na samaki.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akilakiwa na
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Dodoma Balozi Mstaafu Job Lusinde
alipomtembelea nyumbani kwake Uzunguni Mjini Dodoma, Balozi Lusinde
amemuhakikishia Dkt. Mahenge ushirikiano kutoka kwa wazee.

Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akifanya
mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Dodoma Balozi Mstaafu Job
Lusinde alipomtembelea nyumbani kwake Uzunguni Mjini Dodoma, Balozi
Lusinde amemuhakikishia Dkt. Mahenge ushirikiano kutoka kwa wazee.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge wakati Dkt. Mahenge
alipomtembelea Mhe. Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya mji wa
Dodoma.

Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akimtembeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.
Dkt. Binilith Mahenge kwenye mradi wake mpya wa ufugaji samaki wakati
Dkt. Mahenge alipomtembelea Mhe. Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya
mji wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment