
Wakati michezo ya Kimataifa kwa upande wa timu za taifa zikikamilika wiki hii ,wikiendi hii ligi mbalimbali zinarejea tena kuendeleza moto wake katika kusaka mabingwa wa 2017/2018.
Moja kati ya ligi ambayo itarejea mwishoni mwa juma hili ni ligi kuuVodacom Tanzania Bara VPL ambapo mpaka sasa kinara ni Simba SC wenye alama 19 sawa kabisa na vijana wa chamazi Azam Fc wanaoshikilia nafasi ya pili kwa alama hizohizo 19 tofauti ikiwa ni magoli ya kufungwa na kufunga.
Ijumaa ya leo Nov 17 2017 utapigwa mtanange mmoja kati ya wakulima wa alizeti Singida United dhidi ya Wanapaluhengo Lipuli Fc kutoka mkoani Iringa mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Namfua mkoani Singida .Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote kwa maana ya kujiongezea alama katika msimamo wa VPL kwani timu hizi zinatofauti ya alama moja huku Singida United wakiwa juu ya Lipuli kwa alama 1 ikishika nafasi ya 6 na Lipuli kushika nafasi ya 7 kwa kujikusanyia alama 13.
Huu utakuwa mchezo wa pili wa ligi kuu msimu huu kuchezwa katika uwanja wa Namfua tangu ufanyiwe Marekebisho eneo la kuchezea 'PITCH'' wa kwanza ukiwa ni ule wa Nov 04 dhidi ya Dar Young Afrika mchezo uliomalizika kwa sare tasa na singida untd kufikisha dakika 360 bila ushindi za idi ya kutoa sare katika michezo mitano mfululizo.
Ifuatayo ni Ratiba,msimamo VPL Msimu wa 2017/18.
Friday, 17 Nov | ||||
04:49:43 | ||||
Saturday, 18 Nov | ||||
v | ||||
v | ||||
v | ||||
v | ||||
Sunday, 19 Nov | ||||
v | ||||
v |
|
---|
Msimamo | P | W | D L | F | A | GD Pts | |||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Simba SC | 9 | 5 | 4 | 0 | 21 | 5 | 16 | 19 |
2 | Azam Football Club | 9 | 5 | 4 | 0 | 7 | 2 | 5 | 19 |
3 | Young Africans | 9 | 4 | 5 | 0 | 11 | 4 | 7 | 17 |
4 | Mtibwa Sugar | 9 | 4 | 5 | 0 | 7 | 3 | 4 | 17 |
5 | Tanzania Prisons | 9 | 3 | 5 | 1 | 10 | 7 | 3 | 14 |
6 | Singida United | 9 | 3 | 5 | 1 | 6 | 4 | 2 | 14 |
7 | Lipuli FC | 9 | 3 | 4 | 2 | 7 | 6 | 1 | 13 |
8 | Mbeya City | 9 | 3 | 2 | 4 | 9 | 9 | 0 | 11 |
9 | Ndanda FC | 9 | 2 | 4 | 3 | 5 | 6 | -1 | 10 |
10 | Mbao FC | 9 | 1 | 5 | 3 | 9 | 11 | -2 | 8 |
11 | Majimaji FC | 9 | 1 | 5 | 3 | 6 | 8 | -2 | 8 |
12 | Mwadui FC | 9 | 1 | 5 | 3 | 9 | 14 | -5 | 8 |
13 | Kagera Sugar FC | 9 | 1 | 4 | 4 | 6 | 9 | -3 | 7 |
14 | Njombe Mji | 9 | 1 | 4 | 4 | 3 | 9 | -6 | 7 |
15 | Stand United | 9 | 1 | 2 | 6 | 3 | 11 | -8 | 5 |
16 | Ruvu Shooting | 9 | 0 | 5 | 4 | 3 | 14 | -11 | 5 |
Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.
No comments:
Post a Comment