
Pamoja na kuchelewa kufika lakini
timu ya taifa ya Argentina ilifanikiwa kufudhu kwa fainali za kombe la dunia
zitakazochezwa mwakani nchini Urusi na shukrani zimeuendee Lioneil Messi
aliyewabeba katika mchezo wa mwisho.
Lakini wakati wakijiandaa kushiriki
michuano hiyo ya kombe la dunia, mshambuliaji huyo hatari wa klabu ya Barcelona
tayari kichwani ana orodha ya timu ambazo anaamini zitakuwa tishio kwenye
michuano hiyo.
Messi anaamini timu ya taifa ya
Ujerumani ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo ni kati ya timu anazozipa
nafasi kubwa bila kusahau Ufaransa, Brazil na timu ya taifa ya Hispania.
Lakini Lioneil Messi pamoja na
kuzikubali timu hizo lakini kuna timu moja anayoiogopa zaidi nayo ni timu ya
taifa ya Hispania ambayo amekiri kwamba hatamani kabisa kukutana nao katika
michuano hiyo.
Lioneil Messi anaamini kwa sasa timu
ya taifa ya Hispania ndio timu bora na wanacheza vizuri sana hivyo itakuwa
ngumu kupambana nao haswa katika michuano mikubwa kama kombe la dunia.
Kuhusu kufudhu katika michuano hiyo
kwa tabu sana Messi amesema aliamini watakwenda Urusi hata kama itachukua muda
na ndio maana siku ya mchezo aliwaambia wachezaji wenzake watulie wanaelekea
Urusi.
No comments:
Post a Comment