
Serikali ya kata ya Ikomwa katika halmashauri ya Manispaa ya Tabora imewakamata wazazi 12 wa wanafunzi wa shule ya sekondari Ikomwa kwa kusababisha utoro sugu wa watoto wao kwa zaidi ya siku tisini.
Afisa mtendaji wa kata ya Ikomwa Green Biseko amesema serikali ya kata ilipokea taarifa ya utoro wa wanafunzi hao kutoka kwa mkuu wa shule hiyo na kuanza kuwasaka wazazi hao na kuwafikisha katika kituo cha polisi cha kata ya Ikomwa.
”Baada ya kupokea taarifa ya utoro wa hawa wanafunzi kutoka kwa mkuu wa shule ya Sekondari ya Ikomwa ndipo tulipo amua kuchukua hatua za kuwasaka wazazi wao kwa ajiri ya kuwachukulia hatua” amesema Biseko.
Nae Diwani wa kata ya Ikomwa, Salum Msamazi amesema kati ya wanafunzi waliokamatwa,wanafunzi 8 ni wa kidato cha kwanza na wanafunzi wa 5 ni kidato cha pili na kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wazazi hao ili iwe fundisho kwa wazazi wengine.
No comments:
Post a Comment