Manchester United kuendelea kuwachania watu mikeka hii leo? - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 30, 2017

Manchester United kuendelea kuwachania watu mikeka hii leo?


Pamoja na kuondoka kwa Virgil Van Djik lakini Southampton wanaweza kwenda Old Traford hii leo huku wakijiamini, Soton wanajiamini kwa sababu katika mechi 3 za ligi zilizopita Old Traford wameshinda 2.

Lakini kabla ya hapo Southampton walikuwa na wakati mgumu sana katika dimba la Old Traford kwani katika michezo 19 walishindwa kupata matokeo huku wakipigwa michezo 16 na kusuluhu michezo mitatu vs United.

Pamoja na kupata suluhu mbili katika siku za hivi karibuni lakini United sio wakubeza wala kuwachukulia poa kwani katika mechi zao 9 zilizopita za ligi wamepoteza mechi moja tu huku wakishinda 6.

Mashabiki wa United wanaweza kukosa raha kama wakishindwa kuipiga Southampton ambayo katika mechi 11 zilizopita imeshinda mara 1 tu ikipigwa mara 6 na kutoka suluhu mara 4.

Na kama leo Southampton wakishindwa kupata ushindi watakuwa wameifikia rekodi yao ya 2004/2005 ya kucheza mechi 10 bila ushindi iliyodumu toka mwezi November 2004 hadi December 2005.

Manchester United wanahitaji sana kushinda mchezo huu wa leo kwani itawaondoa kwenye presha toka kwa Chelsea ambao wamewapita alama moja na pia kupunguza pengo la alama na vinara Manchester City.

No comments:

Post a Comment