Inawezekana kwa kiasi fulani Mwaka 2017 umekuendea vibaya nikimaanisha katika kuyatimiza yale ambayo ulitamani kuwa nayo katika mwaka huu lakini kwa kiasi hujaweza kuyafanyia kazi au umeyafanyia lakini bado hujafikia lile lengo kuu ambalo ulilitamani.
OKULY BLOG inakutia moyo kwamba bado unanafasi ya kuanza tena kwa sababu moja kati ya dhambi kubwa katika ulimwengu huu ni kukata tamaa simama tena tazama pale ulipojikwaa alafu anzia hapohapo mwaka 2018 ili kuhakikisha uachi viporo nyuma kwa sababu vitaendelea kukukera kutokana kwamba vilitakiwa uvimalizia.
Moja kati ya waandishi wakubwa wa vitabu Duniani Mahatma Gandhi alishawahi kusema "Never allow somebody to walk in your mind with his/her dirty feet" akimaanisha kwamba "Usije ukamruhusu mtu kutembea katika fahamu zako kwa miguu yake michafu" .
Hivyo OKULY BLOG inakushauri usikubali mtu kukukatisha tamaa pambana kwa sababu kukatishwa tamaa ni sawa na mtu kutembea kwenye akili yako na miguu yake michafu hivyo kataa kata kata kukatishwa tamaa ni dhambi ambayo mwisho wake utatupwa motoni na umaskini itakuwa bega kwa bega na wewe kwa sababu kila utakachokijaribu kukifanya unakata tamaa.

OKULY BLOG inaamini kwamba mwaka wa 2017 umekwisha bado siku chache sana hivyo usijute tena kwa kutofanikisha malengo yako waza kuelekea 2018 ukiamini kwa ndoto na malengo yako yanakwenda kukamilika pambana usiku na mchana kutetea maisha yako kwa sababu yapo kwenye viganja vya mikono yako ni wewe tu kuchukua hatua.
Tunakuahidi kwamba mwaka 2018 OKULY BLOG itakuwa karibu yako zaidi kwa matukio mbalimbali ya Kijamii,kisiasa,kiuchumi,Kielimu na burudani na michezo.
Kwa matangazo madogo na makubwa wasiliana na OKULY BLOG kwa simu namba zifuatazo
0769087415 AU 0628914950
Au barua pepe OkulyJulius@gmail.com
Tangaza nasi hakika mabadiliko katika biashara yako yataonekana Biashara ni Matangazo hivyo kuelekea 2018 tangaza biashara yako kupitia OKULY BLOG always we ara PROPER .
2018 uwe mwaka wa mafanikio kwako msomaji wa Tovuti yetu.
Okulyblog.blogspot.com
No comments:
Post a Comment