
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari
17, 2018 amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za
Serikali za msingi na Sekondari na kuwaagiza Mawaziri Jafo na Ndalichako
kusimamia hilo.
Magufuli amepiga marufuku hiyo hiyo leo alipokutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam na kuwataka mawaziri hao kwenda kusimamia jambo hilo na kuhakikisha hakuna michango yoyote wanafunzi au wazazi wanachangishwa kwenye shule za sekondari.
No comments:
Post a Comment