Rais Joe Biden wa Marekani amewasili mjini Rome, akiwa anaanza ziara yake yenye lengo la kurejesha utambulisho wa Marekani katika uso wa kimataifa.
Baadae leo, Biden atakutana na kiongozi wa kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis mjini Vatican na kisha kuzungumza na wawakilishi wa serikali ya Italia.
Siku ya Jumapili, Biden atashiriki mkutano wa kilele wa siku mbili wa kundi la mataifa yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi, G20, mjini Rome, huku China ikisema itashiriki kwa njia ya video.
Jumatatu, Biden anatarajiwa pia kushiriki kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP26, Glasgow, Scotland. Hii ni ziara ya pili ya kimataifa ya Biden tangu alipoingia madarakani, Januari mwaka jana.
No comments:
Post a Comment