MKUU WA WILAYA AMWAMURU DEREVA WAKE ALIPE FIDIA AJALI YA KUUA KIFARANGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 15, 2021

MKUU WA WILAYA AMWAMURU DEREVA WAKE ALIPE FIDIA AJALI YA KUUA KIFARANGA



Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Paul Chacha alilazimika kusimamisha Msafara baada ya Dereva wake Alfred Chaki kugonga Kifaranga katika Kijiji cha Makingi alipokuwa anaendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.


Mkuu huyo wa Wilaya alimuamuru dereva wake alipe fidia ya Shilingi “Elfu Tano” na alikemea tabia ya Madereva kugonga Kuku, Bata, Kanga au Mnyama wa aina yeyote na kisha kuondoka.


Aidha, alisisitiza wananchi walime na kufuga kisasa ili wajikwamue kiuchumi.


Mkuu wa Wilaya Chacha pia aliwaomba radhi akina Mama waliokuwa eneo la tukio na walimshukuru na kumpa baraka za kuendelea na Safari


No comments:

Post a Comment