Upigwaji kura utafanyika katika vituo vilivyotumika wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na Vituo vitafunguliwa saa moja kamili (1:00) Asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10:00) jioni .
![]() |
Afisa habari mkuu wa tume ya taifa ya uchaguzi Bw .BATHELOMEO WANDI akizungumza katika kipindindi cha MORNING BOOSTER cha 97.7 Nyemo fm radio Dodoma. |
Akizungumza katika kipindi cha MORNING BOOSTER cha 97.7 Nyemo fm radio Dodoma kuelekea uchaguzi huo Afisa habari mkuu wa tume ya taifa ya uchaguzi Bw .BATHELOMEO WANDI amesema kuwa wananchi watatakiwa kuhakiki majina yao kwenye mbao katika vituo vyote ambao vitatumika katika upigaji kura na uhakiki huo utafanyika siku nane kabla ya siku ya uchaguzi hivyo itawasaidia wale ambao hawatakuta majina yao kutatua changamoto hiyo kabla ya tarehe ya uchaguzi.
Pia ameongeza kuwa kwa wala waliopoteza ama kuharibika kwa vitambulisho vyao vya kupigia kura wasisite kufika siku ya uchaguzi kwa sababu wataruhusiwa kupiga kura ila ni muhimu wakafika na mojawapo ya vitambulisho vifwatavyo ambavyo ni Hati ya kusafiria,Leseni ya Udereva na kitambulisho cha uraia ambacho majina yote matatu yanafanana na majina yaliyopo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Bw.BATHELOMEO WANDI amefafanua kuhusu uchaguzi mdogo ubunge katika jimbo la Ngorongoro kuwa mpaka sasa vyama zaidi ya 10 vimeshathibitisha kushiriki katika uchaguzi huo na kwa upanda wa uchaguzi mdogo wa udiwani awali zilikuwa kata Saba ila kuna kata mbili ambazo wagombea wake wamepita bila kupingwa ambapo ni kata ya IPWANI iliyopo Mbarali mkoani Mbeya na Bomalang'ombe (Kilolo DC) mkoani hivyo kufanya uchaguzi mdogo wa Udiwani kubaki kata tano (5) pekee ambazo ndizo zitakazofanya uchaguzi siku hiyo.
Pamoja na hayo amewataka wananchi kuzingatia sheria,kanuni na tara6ibu za uchaaguzi ili kuepuka na usumbufu ikiwa ni pamoja na kuhakiki majina yao yaliyotumika katika daftari la kudumu la wapiga kura na kuwataka pia kufuata maelekezo watakayopewa na msimamizi wa kituo ikiwa ni pamoja na kuondoka katika eneo la kituo cha kupigia kura mara baada ya kumaliza kipiga kura.
Bw.BATHELOMEO WANDI amemaliza kwa kusema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi inawakumbusha wapiga kura kuzingatia kanuni za afya kwa kufuata maelekezo watakayopatiwa kituoni ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa wa UVIKO -19 unaosababishwa na virusi vya Korona.
No comments:
Post a Comment