Waziri Ummy ameyasema hayo leo baada ya kupata maelekezo ya kisera kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknojia, Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako ambaye amemtaka kulisisitiza suala hilo ili wanafunzi hao waweze kupata muda wa kupumzika kipindi cha likizo.
Akihutubia kwenye Mahafali ya 29 ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo,Waziri Ummy amesema watoto wanatakiwa kupumzika majumbani kipindi cha likizo ili waweze kusaidia kufanya kazi ndogondogo nyumbani, kusoma dini na kusaidia kufanya biashara ndogo za kuwasaidia wazazi pale wanapokuwa likizo.
“Sasa hivi elimu imegeuzwa kama biashara, watoto wamekuwa wakisoma masomo ya ziada mpaka kipindi cha likizo, hawapumziki, pia wazazi huchangia fedha kwa ajili ya masomo hayo ya ziada, watoto hawafaulu kwa kusoma muda mrefu, hivyo nawaagiza wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanalisimamia hili,” amesisitiza Waziri Ummy.
Amesema, Serikali imepanga muda wa vipindi wa saa nane, ikiamini muda huo wanafunzi wataweza kujifunza kwa kina masomo yote yaliyopangwa kwa siku, hivyo amewataka Wakurugenzi kuwaelekeza wakuu wa shule kusitisha masomo ya ziada mpaka saa mbili usiku Jumatatu hadi Jumapili
"Ninaagiza kusitishwa mara moja kwa kuwa hatuwajengi watoto,tunawaharibu kwa kuwachosha kusoma muda wote bila kupata muda wa kupumzika,"amesema Waziri.
No comments:
Post a Comment