Na Okuly Julius, Dodoma
ZOEZI la uchukuaji fomu za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekamilika hii leo ambapo jumla ya wanachama 71 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka,Katibu msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni ,Solomon Itunda amesema mpaka siku ya mwisho ya uchukuaji fomu waliojitokeza ni wagombea 71 lakini wawili kati yao wameshindwa kurudisha fomu.
Majina ya waliochukua fomu kwa ujumla ni Samweli Mageto, Rahimuddin Ismail, Alex Msama, Themistocles Rwegas na Grangany Nyalohaha.
Aidha wengine waliochukua fomu ni Katibu wa zamani wa Bunge Dk Thomas Kashilila, Waziri wa mifugo wa zamani Luhaga Mpina, Hatibu Madata Mgeja, Dk Linda Ole Saitabau, Profesa Norman Sigara King,Emmanuel Sendama,Dk Thomas Kashilila, Goodluck Milinga, Bibie Msumi, Hilal Seif na Athumani Mfutakamba.
Wengine ni Mwenda Burton Mwenda, Herry Kessy Josephat Malima, Adam Mnyavanu, Stella Manyanya na Andrew kevela.
Pia wamo Luhaga Mpina na Hussein Mataka, Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Msalala Mkoani Shinyanga Ezekiel Maige,, Wakili Emmanuel Mng'arwe, Aziz Mussa, Wakili Onyango Otieno, Doto Mgasa, Profesa Edison Lubua, Fikiri Said, Dkt. Itikija Mwanga na Peter Mjemu.
Ndurumah Mejembe, Godwin Maimu, Johnson Japhet, Mohamed Mmanga, Esther Makazi, Mariam Moja, Joseph Anania, Samweli Xaday, Arnold Peter na Joseph Sabuka.
Wengine ni mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa zamani wa Bariafi Andrew Chenge na Dk Titus Kamani.
Dkt. Mussa Ngonyani, Wakili Faraji Rushagama, Hamisi Rajabu, Dkt. Titus Kamani na Asia Abdallah ambaye amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Kilolo.
Wengine ni Festo Kipate, George Nangale, Barua Mwakilanga, Zahoro Haruna, Andrew Chenge, Thomas Kirumbuyo ,Angelina John na Mhandisi Abdilaziz Jaaf Hussein . Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, Emmanuel Mwakasaka Mbunge wa Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na Profesa Hadley Mafwenga ambaye ni Ofisa usimamizi wa fedha kutoka Wizara ya Fedha Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma,Goodluck Ole Madeye, Sophia Simba,Juma Hamza Chum na Baraka Byabyato.
Pia Simon Ngatunga, Tumsifu Mwasamale, Merkion Ndofi,Dk Tulia Ackson, Godwin Kunambi na Ambwene Kajula,Petrick Nkandi, Steven Masele na Hamidu Chamami.
Baada ya kupata wagombea wote 71 na kati ya hao 2 wameshindwa kurejesha fomu zao zoezi linalofuta kwa hao 69 waliorejesha fomu zao ni kufanyiwa tathmini kila mmoja mpaka atakapopatikana mmoja kati yao atakayewakilisha Chama cha mapinduzi katika kuwania nafasi hiyo ya
U-spika wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mchakato huo unafanyika kufuatia kujiuzulu kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai Januari 6, mwaka huu.
![]() |
Ndugu Hatibu Madata Mgeja akikabidhiwa fomu ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania. |
No comments:
Post a Comment