ALIYEWAHI KUWA MKUU WA WILIYA YA KILOLO BI.ASIA ABDALLAH AJITOSA KUWANIA NAFASI YA U-SPIKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 15, 2022

ALIYEWAHI KUWA MKUU WA WILIYA YA KILOLO BI.ASIA ABDALLAH AJITOSA KUWANIA NAFASI YA U-SPIKA


Bi.ASIA ABDALLAH ambaye amewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoni iringa akikabidhi fomu za kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitiaChama cha  Mapinduzi kwa Mkuu wa Idara ya uchaguzi CCM Ndugu Cuthbert Midala



Bi.ASIA ABDALLAH ambaye amewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoni iringa akiwa ameshikilia fomu za kuwania nafasi ya Spika kupitia chama cha Mapinduzi

Mambo yanaendelea kupamba moto katika zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi ya Spika  wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ambapo makada mbali mbali wanaendelea kujitokeza kutimiza haki yao hiyo ya kikatiba kupitia chama cha mapinduzi.

Mmoja wa makada walioyochukua fomu na kurejeshi ni
Bi.ASIA ABDALLAH ambaye amewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoni irinnga huku akisema kuwa amejipima na kuona kuwa anatosha kukalia kiti hicho endepo atafanikiwa kupenya katika mchakato huo.


Bi.ASIA ABDALLAH amesema kuwa amevutiwa na kushawishika na kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutaka vijana wachakamkie nafasi za kiuongozi zinazojitokeza ili kuleta mawazo chanya na kisasa katika kuongoza serikali kupitia muhimili huo wa bunge.

Ameongeza kuwa ni wakati wa vijana kujitokeza kwa ajili ya kuisaidia serikali katika ngazi za uongozi na ndio maana ameamua kujitosa katika nafasi hiyo iliyopo wazi baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kujiuzulu.

"Nimejipima,najiamini na Nina uzoefu wa kutosha katika uongozi hivyo nafasi hii endapo nitafanikiwa kushinda nitamsaidia Rais katika kutekeleza mipango yote ya maendeleo na yenye tija kwa wananchi"" amesema Bi.ASIA ABDALLAH.


Bi.ASIA ABDALLAH ambaye amewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoni iringa akikabidhi fomu za kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitiaChama cha  Mapinduzi kwa Mkuu wa Idara ya uchaguzi CCM Ndugu Cuthbert Midala


Ikumbukwe tu kuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni january 15,2022 saa kumi kamili jioni hivyo kama bado ujachukuwa fomu muda bado upo kikubwa ni kufika katika ofisi kuu za Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma ,Ofisi ndogo Dar es salaam, na Afisi kuu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment