Hayo yamesemwa hii leo tarehe 14 ,Januari 2022 na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni Solomon Itunda wakati akitoa takwimu za siku ya leo ya wanachama waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo.
Amesema kuwa katika vituo vitatu ambavyo vimetengwa kwa ajili ya zoezi la uchukuaji fomu ambapo ni Makao makuu ya CCM jijini Dodoma kwa siku ya leo wamejitokeza wanachama 3 ,kwa upande wa ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam ni 12 na kwa upande wa Afisi kuu Zanzibar wamejitokeza wanachama 2.
Hivyo kufanya Idadi ya wanaowania nafasi hiyo kwa siku ya leo kuwa ni 17 ambapo kwa idadi hiyo inafanya mpaka sasa wagombea wanaowania nafasi ya Spika la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi ni 66 na zoezi Hilo litakamilika kesho majira ya saa kumi kamili jioni hivyo bado kuna fursa kubwa kwa wanachama wengine kuchukua na kurejesha fomu.
Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni Solomon Itunda ameendelea kuwakumbusha na kuwahamasisha wanachama wenye nia kuendelea kujitokeza ili kupata haki hii ya kikatiba.
Ikumbukwe tu kuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni january 15,2022 saa kumi kamili jioni hivyo kama bado ujachukuwa fomu muda bado upo kikubwa ni kufika katika ofisi kuu za Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma ,ofisi ndogo za Dar es salaam, na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment