Zoezi Hilo la kuchukuwa fomu Amelifanya hii leo katika ofisi kuu za CCM mkoani Dodoma na ameelezea dhamira yake ya kuwania nafasi hiyo kuwa ni kutimiza takwa la kikatiba la chama chake na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akiahidi kuisaidia serikali kutimiza malengo yake kupitia muhimili wa bunge.
Ameongeza kuwa kilichomshawishi zaidi kujitosa katika nafasi hii ya Uspika ni hamasa aliyoipata kutoka kwa Raisi Samia Suluhu Hassan ambaye amewataka vijana kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali zinazotokea za kiuongozi.
Amesema kuwa yeye kama kijana atakuwa bega kwa bega na serikali ya Raisi Samia ambayebamekuwa akiwaunga mkono vijana na ameongeza kuwa mbali na kuwa Mhadhiri amekuwa akihamasisha vijana hasa wakike Katika maswala ya Sayansi pamoja na uongozi.
Pamoja na hayo Dr.Linda Peniel Salekwa amesema kuwa kwa kujitokeza kuwania nafasi hiyo ya uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya kwa vitendo na kuwa mfano kwa vijana wa kike na kuwaonesha kuwa hata vijana hasa wa kike wana haki na wajibu wa kuwania nafasi kubwa serikali.
No comments:
Post a Comment