MGEJA:ACHUKUA FOMU YA KUWANIA NAFASI YA SPIKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 14, 2022

MGEJA:ACHUKUA FOMU YA KUWANIA NAFASI YA SPIKA


HATIBU MADATA MGEJA akikabidhiwa fomu mapema hii leo katika ofisi kuu za Chama cha mapinduzi mkoa wa Dodoma


Zoezi la kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado linaendelea huku Makada mbalimbali wakijitokeza kuchukua fomu hizo lengo ni kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa spika wa bunge hilo Job Ndugai aliyejiuzulu mapema mwezi huu.

Ambapo leo katika ofisi kuu za CCM jijini Dodoma amejitokeza mwanachama mwingine Ndugu HATIBU MADATA MGEJA kutaka kutumia haki yake ya kikatiba kuwania nafasi hiyo ya uspika ,Amesema kuwa yeye kama kijana ameguswa kutoa mchango wake katika kulitumikia taifa katika muhimili huo wa Bunge.

Amesema kuwa akifanikiwa katika mchakato huu wa kuwa Spika atalisaidia bunge kwa kuhakikisha wanamsaidia kwa ukaribu Raisi Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza kile ambacho amekusudia kuwafanyia watanzania katika miaka hii mitano.


Ameongeza kuwa hatishwi na majina wa watu wenye ushawishi mkubwa waliojitokeza kuwania nafasi hii kwa sababu kila mmoja ana haki ya kikatiba kichama na kitaifa ya kuwania nafasi hii hivyo baada ya mchakato huu Chama Cha Mapinduzi kitakuwa na kazi ya kupitisha majina ya watakaokwenda kupigiwa kura kwa ajili ya kupata mtu wa kuliongoza bunge.

MGEJA amekumbusha kuwa nchi yetu ilipopata uhuru baraza la kwanza la mawaziri lilikuwa limejaa vijana hivyo yeye kama kijana anaamini kuwa vijana wana fikra za kisasa na amempongeza raisi kwa kuendelea kuwahamasisha vijana kujitokeza katika nafasi mbalimbali za uongozi zinazotangazwa na serikali.

Ikumbukwe tu kuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni january 15,2022 saa kumi kamili jioni hivyo kama bado ujachukuwa fomu muda bado upo kikubwa ni kufika katika ofisi kuu za Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma ,Dar es salaam, na Zanzibar.

MGEJA ni zao la chama cha Mapinduzi kwani katika elimu yake Chuo kikuu Cha Dar es Salaam katika fani ya Siasa ,uongozi na mahusiano ya kimataifa na huko nchini Norway amesomeshwa na CCM hivyo amejipima vya kutosha ndio maana ameamua kujitosa katika kuwania nafasi hii ili kushiriki utumishi wake katika muhimili huu wa bunge.



No comments:

Post a Comment