Hatua ya kuchukua fomu inatokana na nafasi hiyo kuwa wazi baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo na Mbunge wa Kongwa Job Ndugai kujiuzulu.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo Maige amesema kuwa ana historia nzuri kwa chama chake ambapo alijiunga akiwa na umri wa miaka 19 hivyo ana uwezo wa kukiwakilisha vema katika kuleta maendeleo ya nchi hasa katika kupambana na Umaskini, Ujinga na Maradhi.
Maige amesema ana uzoefu katika uongozi na Bunge hilo kwa kuwa alilitumikia kwa zaidi ya miaka 13 na kwamba anauzoefu mkubwa na wabunge kiutendaji.
Maige ameeleza kuwa lengo kuwania nafasi hiyo ni kutekeleza haki ya kikatiba ya chama cha CCM ikiwemo za kuitumikia nchi na watu wake na kujitolea kwa nafasi kuondoa umaskini.
“Kama mwanachama nitatekeleza ahadi zote na endapo nitafanikiwa katika hili naahidi kutoa ushirikiano katika Bunge hususan kwenye mambo ya sheria," amesema Maige.
No comments:
Post a Comment