HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAMUANDALIA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ZAWADI ATAKAPOTIMIZA MWAKA MMOJA AKIWA MADARAKANI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 13, 2022

HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAMUANDALIA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ZAWADI ATAKAPOTIMIZA MWAKA MMOJA AKIWA MADARAKANI.



Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akizungumza katika ziara yake ya kukagua maendelea ya ujenzi ya Machinga Complex Dodoma

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Fatma Mganga, akizungumza katika ziara hiyo na kusema kuwa halmashauri ya jiji la Dodoma inastahili pongezi kwa hatua hii


MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka ameitaka Kampuni ya Mohammed Bulders inayojenga eneo la Wamachinga katika eneo la Bahiroad Jijini hapa kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa mradi huo ifikapo March 17 mwaka huu ili kumpa zawadi Rais Samia Suluhu Hassan ya kutimiza mwaka mmoja tangu awe madarakani.

Hayo yameelezwa leo,Januari 13,2022 na Mkuu huyo wa Mkoa wakati alipofanya ziara katika eneo hilo ambapo amesema sababu ya kutaka ujenzi wa eneo hilo ukamilike March 17 ni kutokana na Rais Samia siku hiyo kufikisha mwaka mmoja tangu akiwa madarakani.

Katika ziara hiyo,Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa ameongozana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Fatma Mganga,Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,Joseph Mafuru,Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa,wataalamu kutoka Jiji la Dodoma na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Pamoja na hayo Mtaka amewataka watumishi wa halmashauri ya jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa wamachinga wote wanasajiliwa katika mfumo wa kielectroniki ili kuepusha janjajanja ya mtu mmoja kujirudia zaidi ya mara moja.


Pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Halmashauri ya jiji la Dodoma kwa kuwa kielelezo kati halmashauri 184 nchi nzima kwa kuweza kutumia mapato yake ya ndani kufanya jambo kubwa ambalo ni la kuigwa na halmashauri zingine.

Mtaka amependekeza na kuwashauri wamachinga kuwa wajitahidi pindi wanavyopata nafasi ya kufanya biashara katika MACHINGA COMPLEX wahakikishe hawachui muda mrefu na wafanye jitihada za kuwa wafanyabiashara wakubwa ili waweze kuwaachie wengine wanaochipukia.

"Hakuna sababu ya mtu kupangisha kibanda kwa muda mrefu kutakuwepo na muda maalumu ambao utapendekezwa wa mtu kumiliki kibanda baada ya muda huo tunaamini machinga huyo ameshakuwa na kuachia kibanda kwa mtu mwingine na hatupangishi vibanda vya kudumu"Amesema Anthony Mtaka mkuu wa mkoa wa Dodoma

Kwa upande wake,Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Mganga amelipongeza Jiji la Dodoma kwa kutenga asilimia 40 ya mapato ya ndani kuweza kujenga eneo hilo la wajasiriamali kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7.5 huku akizitaka Halmashauri zingine za Mkoa huo kuiga mfano wa Jiji la Dodoma.

Dk.Mganga ameongez kuwa halmashauri ya jiji la Dodoma imejizatiti kikamilifu kuhakikisha kuwa MACHINGA COMPLEX inakamilika kwa kutumia mapato ya ndani,huku akisema kuwa haya yote yanayofanika katika halmashauri ya jiji la Dodoma ni jitihadi za kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani katika miradi ya maendeleo.

Amekazia pia swala la uzalendo katika kusajili wamachinga wenye sifa ya kuwa na eneo la kufanyia biashara zao huku akiwatoa hofu kuwa hakuna upendeleo wowote katika kuwapatia vibanda wamachinga.

Awali Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa DODOMA Bruno Mponzi akaahidi kusimamia mchakato wa kusajili wamachinga ili kupata idadi husika pamoja na watu sahihi na si vinginevyo.


Eneo la MACHINGA COMPLEX linakadiriwa kuwa na mita zaidi ya 400 ambapo itakuwa BLOCKS 8 kuanzia Block A mpaka F na kila block itakuwa na idadi yake ya Stores na inakadiriwa kuwa itakuwa na uwezo wa kubeba Wamachinga 3000 kwa awamu ya kwanza ila nia na malengo ni kuweza kubeba machinga zaidi ya 5000.

Zaidi ya yote ni pongezi kwa halmashauri ya jiji la Dodoma kwa kudhubuti na kuweza kuanzisha ujenzi wa MACHINGA COMPLEX kwa mapato yao ya ndani bila kuomba msaada popote.






No comments:

Post a Comment