WAZIRI MKENDA KUTENGA MUDA WA WIKI TATU KUZUNGUNZA NA WATUMISHI WA WIZARA YA ELIMU ,SAYASI NA TEKNOLOJIA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 13, 2022

WAZIRI MKENDA KUTENGA MUDA WA WIKI TATU KUZUNGUNZA NA WATUMISHI WA WIZARA YA ELIMU ,SAYASI NA TEKNOLOJIA.



Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda atatenga muda wa wiki tatu kuzungunza na watumishi wa wizara hiyo ikawa ni pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali muhimu kwa lengo la kufanya uchambuzi yakinifu kwa ajiili ya kuboresha elimu iwe na tija.

Profesa Mkenda ameyasama hayo mapema leo tarehe 13/01/2022 jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako.

Hayo yamejiri baada ya mabadiliko baraza la mawaziri yaliyofanywa na Raisi Samia Suluhu Hassan kwa baadhi ya wizari hivi karibuni ambapo Profesa Mkenda amehamishiwa katika wizara hiyo akitokea wizara ya Kilimo na aliyyekuwa waziri wa elimu , sayansi na teknolojia Profesa Ndalichako yete akihamishiwa katika Wizara ya nchi,Ofisi ya Waziri mkuu,kazi,ajira,vijana na wenye ulemavu.



Profesa Mkenda amesema kuwa wizara hiyo ni nyeti hivyo inahitajika kufanya kazi kwa kushirikiana na watumishi na hiyo ndio njia nzuri ya kuitendea haki wizara hiyo.

"Wizara hii ni nyeti sana hivyo hatupaswi kubadilisha badilisha mambo kwani tukifanya hivyo tutalichanganya taifa" Amesema Profesa Mkenda ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Rombo mkoni Kilimanjaro.

"Ili kufanya kazi vizur niwaombe ushirikiano wenu na msiwe na nidhamu za woga mkiona mambo hayaendi vizuri msisite kusema kwani nyie ni wazoefu katika wizara hii" Amesema Profesa Mkenda

Profesa Mkenda ameongeza kuwa ili kufanikiwa katika kazi yeyote ni lazima kufanya kazi kwa timu na kutowa uhuru kwa watumishi wa wizara hiyo kumfuata na kumuelekeza.

Sanjari na hayo Profesa Mkenda amesema kuwa ili kuiboresha elimu ya Kitanzania haoni tatizola kushirikiana na wataalamu wa elimu katika nchi hii.

Kwa upande wake Profesa Ndalichako amewasisitiza watumishi wa Wizara hiyo kumpa ushirikiano waziri wao ili kuendeleza wizara hiyo muhimu.

Amesema kuwa anakabidhi wizara hiyo kwa waziri mgeni huku akiamini kuwa atandeleza mipango mbalimbali iliyopo katika wizara hiyo.

"Kwanza kabisa ninawashukuru watumishi we wenzangu wote kwa ushirikiano mlionionesha kwa kipindi chote nikiwa kama waziri wenu na niwaombe pia mshirikiane vyema na waziri mpya kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hili.

No comments:

Post a Comment