NAIBU WAZIRI WA NISHATI, WAKILI STEPHEN BYABATO(MB). AMEELEZA KURIDHISHWA NA HALI YA UPATIKANAJI WA MAJI KATIKA BAADHI YA MABWAWA YANAYOTUMIWA KUZALISHA UMEME LIKIWEMO BWAWA LA KIHANSI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, January 26, 2022

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, WAKILI STEPHEN BYABATO(MB). AMEELEZA KURIDHISHWA NA HALI YA UPATIKANAJI WA MAJI KATIKA BAADHI YA MABWAWA YANAYOTUMIWA KUZALISHA UMEME LIKIWEMO BWAWA LA KIHANSI.




Watanzania hususani wanaoishi kando ya mito inayoingiza maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme kote nchini wamehimizwa kulinda na kutunza mazingira na vyanzo vya maji ikiwemo kuacha uchomaji ovyo moto na kufanya kilimo kisicho rafiki kwa mazingira ili upatikanaji wa maji uwe ni wa uhakika zaidi wakati wote.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Stephen Byabato, amesema hayo wakati akikagua na kujionea maendeleo ya uzalishaji umeme kwenye mgodi wa kufua umeme wa Kihansi uliopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro ambao una uwezo wa kuzalisha megawatts za umeme 180 kwa wakati mmoja katika mitambo mitatu iliyopo.


Byabato amesema bwawa la kuzalisha umeme la Kihansi lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawatts 180 iwapo maji yatakuwepo kwa wingi wa mita 1,141 juu ya usawa wa bahari ambapo kina kikijaa huwa na uwezo wa mita 1,146, na sasa kutokana na mvua zilizonyesha, bwawa hilo limefikisha mita 1,145 ikiwa bado mita moja tu ifike ujazo wa juu wa mita katika bwawa hilo.

Akawaonya wananchi wanaoishi jirani na mabwawa kuacha kufanya shughuli hatarishi na zisizo rafiki na mazingira ikiwemo uchomaji ovyo moto na kilimo kisicho rafiki na kusababisha maji yanayoingia katika mabwawa kupungua na kusababisha madhara makubwa, licha ya kufahamu umuhimu wa mabwawa hayo yanayowafaidisha hata wao ikiwemo kuwapatia umeme wa uhakika.

Pia amewahimiza viongozi wa kijamii na kiserikali kushirikiana na wananchi kulinda na kutunza vyanzo vya maji ikiwemo misitu na mazingira ingawa bado kuna vyanzo vingine vya uhakika vya umeme ikiwemo gas ambayo Serikali inaendelea kuboresha kwa kufanya mazungumzo na wataalamu na wawekezaji zaidi ili kuzalisha ya kutosha.






#WizarayaNishati
#Kaziiendelee


No comments:

Post a Comment