TAKUKURU DODOMA YAANZA KUTEKELEZA MKAKATI WA KUWAELIMISHA VIJANA KUHUSU MAPAMBANDO DHIDI YA RUSHWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 20, 2022

TAKUKURU DODOMA YAANZA KUTEKELEZA MKAKATI WA KUWAELIMISHA VIJANA KUHUSU MAPAMBANDO DHIDI YA RUSHWA



Na ,Okuly Julius Dodoma 
Ili kuhamasisha ushiriki wa jamii katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa ,Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Dodoma imeanza kutekeleza mkakati wa kuwaelimisha vijana ambao ni wanachama wa SKAUT na waliopo kwenye klabu za wapinga rushwa kuhusu nafasi zao ili kuzuia vitendo vya rushwa katika jamii wanamoishi.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa taasisi hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari’’ Lengo ni kuwa na watumishi wa sekta za umma na binafsi na wananchi kwa ujumla ambao uzalendo wao utawafanya waichukie rushwa ''amesema

Aidha, Kibwengo amesema katika eneo la uelimishaji umma ili kuhamasisha ushiriki wa jamii kwa ujumla katika mapambano dhidi ya rushwa, wamefanya mikutano 47 ya hadhara, semina 90, onesho moja kwa lengo la kuimarisha klabu 121 za wapinga rushwa zilizopo kwenye shule za msingi, sekondari na vyuo.

‘’ Tulishiriki katika vipindi 12 vya redio, baadhi ya mikutano ya hadhara ilifanyika kwa utaratibu wa 'TAKUKURU INAYOTEMBEA' ambapo kwa kutumia gari la matangazo tuliwahamasisha wafanyabiashara kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji wa biashara, kutambua umuhimu na wajibu wa kulipa kodi, kutotoa wala kushawishi kutoa rushwa’’

Katika hatua nyingine ,Kibwengo amesema kwa kushirikiana na wadau wengine, waliweka nguvu nyingi kufuatilia madarasa yaliyojengwa kwa fedha na Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -19  pamoja na madarasa jumla ya miradi 596 yenye thamani ya shilingi (20,660,907) ilikaguliwa.

‘’Ushauri ulitolewa kwa wahusika kuboresha maeneo yaliyokuwa na changamoto’’

Sambamba na hayo ameongeza kuwa wamekamilisha miradi minne iliyokuwa imekataliwa kuzinduliwa na kiongozi maalum wakati wa mwenge wa uhuru mwaka 2021

’’Kati ya miradi hiyo minne, miradi mitatu kati yake ilikutwa na dosari ndogo ndogo, ambazo zilijadiliwa na kurekebishwa lakini kwenye mradi mmoja inaonekana malipo yaliyofanyika bila kazi husika kutekelewa, hivyo tunashirikiana na halmashauri husika kufuatilia marekebisho ya dorasi hiyo’’’

Hatahivyo, Amesema katika kuzuia vitendo vya rushwa ,walifanya chambuzi za mifumo 9 ya utendaji na utoaji huduma katika mkoa wa Dodoma na kushirki warsha 11 za kujadili matokeo ya uchambuzi wa mifumo hiyo. 


No comments:

Post a Comment