UMMMY: "BORESHENI HUDUMA KWA WANANCHI ILI KUPUNGUZA KERO NA MALALAMIKO " - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 17, 2022

UMMMY: "BORESHENI HUDUMA KWA WANANCHI ILI KUPUNGUZA KERO NA MALALAMIKO "


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu


Dodoma,

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amekutana na Viongozi wa Idara ya kinga na kufanya mapitio ya pamoja kuhusu mafanikio ,changamoto na vipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga nchini ili kupunguza maradhi,ulemavu na hivyo kupunguza gharama za matibabu na vifo miongoni mwa watanzania

Kikao hicho kimefanyika mapema leo Januari 17, 2022 katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe.

Katika kikao hicho, Mhe. Ummy amesisitiza juu ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi ili kupunguza kero na malalamiko katika jamii katika nyanja zote, ikiwemo katika huduma za mama na mtoto na huduma za lishe.

Mapitio yaliyofanywa kwenye kikao ni pamoja na ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ,huduma za chanjo,afya ya uzazi na mtoto,huduma za lishe,afya mazingira,Elimu ya Afya kwa Umma.

Aidha, wamejadili mikakati mbalimbali ya mapambano dhidi ya UVIKO-19, Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele(NTDs), Malaria,Kifua Kikuu na Ukoma na UKIMWI.


#AfyaKwanza

No comments:

Post a Comment