Na,Okuly Julius, Dodoma
Hayo yamesemwa hii leo Februari 25,2022 Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi wakati akifunga mafunzo hayo yaliodumu kwa siku tano na kutunuku vyeti kwa wahitimu ambao sasa wana wajibu wa kwenda kuyafanyia kazi yale yote walioyajifunza kwa vitendo.
Pamoja na hayo amesema kuwa makosa ya kimtando imekuwa vita nyingine katika dunia ya sas hivyo kupitia mafunzo haya ni muhimu kwa jeshi la polisi kutumia kwa uweledi mkubwa ili kuendelea kulinda amani ya nchi.
"Tumieni Mafunzo haya mliyoyapata kwa weledi mkubwa lengo likiwa ni kuendelea kulinda amani ya nchi yetu" Amesema Dkt.Jimmy Yonazi
Amehidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuwa wataendelea kuandaa mafunzo ,makongamano na kushirikiana pia na mataifa mengine katika kuongeza na kukuza utaalamu wa namna ya kukabiliana na makosa ya kimtandao.
Aidha Dkt.Jimmy Yonazi ameongeza kuwa suala hili la kupambana na Makosa ya kimtandao ni watu wote sio kuliachia jeshi la polisi wenyewe ni vyema kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie na mwalimu pia katika kukumbushana sheria na taratibu nzuri za matumizi ya mtandao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camilius Wambura amewataka wahitimu wote kuyafanyia kazi mafunzo waliyoyapata kwa ajili ya kuleta tija kwa taifa na wanachi kwa ujumla ,amesema kuwa suala la nidhamu,heshima na kujituma katika kudhibiti makosa haya ya kimtandao itakuwa chachu kubwa kwa jeshi la polisi kwa sababu watakuwa wanatumia akili nyingi na vifaa vya TEHAMA katika kukabiliana na uhalifu wa mitandaoni.
Nao wahitimu wa Mafunzo hayo kwa kauli moja wamesema kuwa watakwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo yale yote waliojifunza huku wakiahidi kuwa wataongeza Weledi zaidi katika kukabiliana na makosa ya kimtandao.
No comments:
Post a Comment