Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Mwanasha Tumbo (kulia) akimkabidhi hati za mashine Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga. |
Na Mwandishi wetu, Dodoma
WIZARA ya afya kwa kushirikiana na wadau wameanzisha mpango jumuishi wa uchanganyaji madini joto kwenye chumvi ili kusaidia wajasiliamali kutengeneza chumvi yenye ubora.
Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wizara ya afya Prof. Abel Makubi jijini Dodoma wakati wa hafla ya Makabidhiano ya Mashine za Kuchanganya Madini Joto kwenye chumvi kati ya katibu mkuu wizara ya afya na katibu mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Prof. Riziki Shemdoe amesema kuwa mashine hizo zitasaidia kupunguza tatito la kutowekwa madini joto ambapo hadi sasa zaidi ya tani zaidi ya laki 1 na 40 zinazozalishwa nchini haziwekwi madini joto.
Nao wadau walioshirikiana katika kufanikisha utengenezaji wa mashine hizo wameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa mashine hizo kutengenezwa hapa nyumbani ambapo gharama kubwa imeokolewa ikilinganishwa na kama mashine hizo zingeagizwa nje. Ambapo zimepunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 50.
Hii ni awamu ya pili kwa mashine hizo kutumika hapa nchini ambapo tayari Mashine 3 tayari zimeshaingizwa nchini kutoka nchi ya Afrika ya Kusini na kunufaisha halmashauri 3.
Mashine 5 za kuchanganya chumvi na madini joto zilizoundwa na VETA kwa ghara ya sh. mil 55.Kila moja imegharimu sh. mil. 11. Awali mashine kama hiyo ilinunuliwa Afrika Kusini kwa sh. mil 25, hivyo kwa kila moja imeokolewa sh. mil 14.
No comments:
Post a Comment