![]() |
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa Dr.Alfonce Chandika aliyesimama |
Dr.Alex Kimambo ambae ni Daktari bingwa wa kinywa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa. Aliyesimama
Dr.Goerge Dilunga yeye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa. aliyesimama
![]() |
Ndg.Jeremia Mmbwambo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa. Aliyesimama |
*****************
Na,Okuly Julius, Dodoma
Hayo yamejiri wakati akiutambulisha ugeni wa hospitali hiyo bungeni mkoani.
Mh.Spika amesema kuwa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma bora na za kibingwa kwa watanzania wote wanaofika hospitalini hapo.
Pamoja na hayo Mh. Dr.Tulia amewapongeza kwa kutoa huduma kwa Waheshimiwa Wabunge na watumishi wa bunge huku akisema kuwa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wabunge pindi wanapohudhuria huduma za kiafya hospitalini hapo.
"Waheshimiwa wabunge hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa imetenga eneo maalum kwa ajili yenu hivyo mkifika pale katika hospitali yetu hii kubwa wewe ulizia tu vijana watakuonesha na vijana wapo pale wanafanya kazi nzuri sana" Amesema Mh.Dr.Tulia Ackson
Ugeni wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa umeongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dr.Alfonce Chandika wengine ni Dr.Alex Kimambo ambae Daktari bingwa wa kinywa, Dr.Jasinta Fex ambaye ni daktari bingwa wa Macho,Dr.Goerge Dilunga yeye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya dharura,Dr.Ernest Masanja ambae ni daktari bingwa wa masikio,pua na koo,Fransisca Gilo ambaye ni Muuguzi pamoja na Ndg.Jeremia Mmbwambo ambae ni Msemaji wa hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment