DKT CHUWA :NCHI ZA AFRIKA ZIMEENDELEA KUDURUFU[KU –COPY NA KU-PASTE ]KUTOKA TANZANIA MFUMO WA SENSA WA KUSHIRIKISHA ZAIDI WALIMU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 19, 2022

DKT CHUWA :NCHI ZA AFRIKA ZIMEENDELEA KUDURUFU[KU –COPY NA KU-PASTE ]KUTOKA TANZANIA MFUMO WA SENSA WA KUSHIRIKISHA ZAIDI WALIMU.



Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu[NBS]Dkt.Albina Chuwa akizungumza na Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa Elimu kata kutoka katika jiji la Dodoma

Afisa elimu mkoa wa Dodoma Gift Kyando akifungua mafunzo juu ya Sensa ya watu na makazi 2022 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma


Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Zanzibar,Balozi Mahammed Hamza

*********************
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu[NBS]Dkt.Albina Chuwa amesema asilimia kubwa ya nchi za Afrika zimeiga [ku-copy na ku-paste]mfumo wa sensa wa kushirikisha Zaidi walimu katika zoezi hilo.

Dkt.Chuwa amebainisha hayo leo Februari 18,2022 jijini Dodoma wakati wa utoaji mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa Elimu Mkoa wa Dodoma katika uhamasishaji kwa jamii katika ushiriki wa sensa ya watu na makazi zoezi litakalofanyika Mwezi Agosti mwaka huu.

Dkt.Chuwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Masuala ya takwimu barani Afrika amesema nchi nyingi za Afrika zimeendelea kuiga na kupata uzoefu wa Tanzania katika kuendesha masuala ya sensa hasa kwa kutumia walimu wa msingi kuwa makalani na wasimamizi wa sensa.

“Mimi ni mwenyekiti wa Bara la Afrika Masuala ya Takwimu,kwa hiyo nchi nchi nyingi za Afrika zimeendelea ku-Copy na ku-paste kutoka Tanzania masuala ya uendeshaji zoezi la sensa kwa kuwatumia walimu ,zoezi letu la sensa tutaendelea kuwashirikisha ikiwemo kutoa mafunzo ,na safari hii hatutumii tena karatasi ,unamaliza mtu wa mwisho kuhesabu sisi tunajua idadi makao makuu muda huohuo”amesema.

Aidha,Dkt.Chuwa amesema kundi la walimu ni kundi muhimu katika kuhamasisha wanafunzi na jamii kwa ujumla katika ushiriki wa sense huku akizungumzia umuhimu wa sensa ni pamoja na kupata takwimu sahihi kwa ajili mipango ya taifa kuleta maendeleo.

“Ni mara ya kwanza kukutanisha kundi la walimu mkoa wa Dodoma na kuwaelezea umuhimu wa sensa,akina mama mnafahamu huwezi ukachota mchele ukapika kilo ishirini kama una watu wawili nyumbani ,hata mama zetu mama Ntilie ni lazima aangalie nini nikaweke wapi hii biashara yangu ,na yeye anahitaji takwimu hizi”amesema.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Zanzibar,Balozi Mahammed Hamza amesema ni wajibu muhumu kwa walimu kuwatumia wanafunzi kuwafundisha kuhusu sensa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema walimu ni mwanga muhimu kwa jamii hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kuwajengea uwezo.

“Sisi kama mkoa tumeona walimu ni mwanga muhimu kwa jamii hivyo wakijengewa uwezo wakaelewa itasaidia sana katika uhamasishaji suala la sense”amesema.

Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa ,afisa elimu mkoa wa Dodoma Gift Kyando ameitaka ofisi ya Taifa ya Takwimu kufika katika halmashauri nyingine kutoa mafunzo ya umuhimu wa sense ili kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ikiwemo maafisa elimu,pamoja na walimu.

Ikumbukwe kuwa Tanzania hushiriki zoezi la sensa kila baada ya miaka 10 na sensa ya mwaka huu itakuwa ni sensa ya 6 na inatajwa ni kwa mara ya kwanza itafanyika kwa kidijitali na zoezi hili muhimu likitarajiwa kufanyika Mwezi Agosti na tarehe itapangwa na mamlaka husika.

Washiriki wa mafunzo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022


No comments:

Post a Comment