Na ,Okuly Julius, Dodoma
Tume ya nguvu za atomiki Tanzania [TAEC]kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara wamekaa kikao cha Pamoja cha kupitia mapendekezo ya marekebisho na maboresho ya Kanuni za tozo .
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Dkt.Alexander Mtawa amesema kikao hicho kitasaidia kuleta maboresho ya kanuni za nguvu za atomiki nchini.
Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania[TAEC]Prof.Lazaro Busagala amebainisha malengo ya kikao hicho ni pamoja kujadili namna ya kuwalinda wananchi wasidhurike na madhara yatokanayo na mionzi.
Pamoja na hayo Prof.Lazaro Busagala ameongeza kuwa wafanyabiashara wadogo hawatokuwa wanalipa tozo na badala yake watakuwa wanapata huduma kwa ubora uleule.
Hata hivyo amewataka wafanyabiashara kujisajili katika Tume ya nguvu za atomiki Tanzania (TAEC) ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo yao ikiwa ni ndani na nje ya nchi.
Akiwahakikishia Watanzania kuwa mpaka sasa hakuna tukio lililoripotiwa la madhara yatokanayo na mionzi kwa sababu Tume hiyo ipo makini katika kuhakikisha usalama wa Watanzani katika nyanja hiyo ya mionzi.
Mmoja wa wadau hao,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya usafirishaji wa bidhaa Tanzania Exporters Association [TANEXA ]Peter Lanya amezungumzia manufaa watakayopata kutokana na maboresho ya kanunihizo,ikiwemo urahisishwaji katika usafirishaji wa mizigo kwa upande wao kama wafanyabiashara itawasaidia sana.
Ikumbukwe kuwa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania[TAEC]ilianzishwa kwa sharia ya Bunge Na.7 ya mwaka 2003 na hapo awali ilikuwa ikijulikana kama Tume ya Taifa ya Mionzi iliyoanzishwa kwa sharia ya Bunge Na.5 ya mwaka 1983 na miongoni mwa majukumu yake ni kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini,kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya Teknolojia ya Nyuklia na kufanya utafiti na kutoa ushauri na taarifa mbalimbali juu ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia.
No comments:
Post a Comment