WAHAMIAJI HARAMU 45 RAIA WA ETHIOPIA WAISHIA MIKONONI MWA JESHI POLISI MKOANI DODOMA, WALIKUWA WANASAFIRISHWA UGHAIBUNI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, February 13, 2022

WAHAMIAJI HARAMU 45 RAIA WA ETHIOPIA WAISHIA MIKONONI MWA JESHI POLISI MKOANI DODOMA, WALIKUWA WANASAFIRISHWA UGHAIBUNI









Na,Okuly Julius, Dodoma 
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 53 wakiwepo wahamiaji haramu 45 Raia wa Ethiopia waliokamatwa katika Milima ya Kolo wakipumzika kwa ajili ya kuendelea na safari kuelekea ughaibuni.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amasema kuwa wahamiaji hao haramu wamekamatwa na Askari waliokuwa doria tarehe 11,February 2022 .


Kamanda Lyanga ameongeza kuwa wahamiaji wote hao haramu watafikishwa mahakamani mapema baada ya majalada yao kukamilika huku akitoa rai kwa raia wa Tanzania kuacha kushiriki katika usafirishaji wa Raia wa kigeni ambao hawafuati utaratibu wa kisheria wa kuingia nchi nyingine zaidi sana wanatumia njia za magendo.



Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Uhamiaji ambaye ndio Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Bahati Jonathan Mwaifuge amesema kuwa mpaka sasa Mkoa wa Dodoma una wahamiaji haramu takribani 158 ambapo kati yao kuna Waethiopia 145,Wasomali 9 na Wapakistani 4 ambao baadhi yao kesi zao zimeshafikishwa mahakamani.

Ameongeza kuwa wapo macho na hawawezi kumvumilia mtu yeyote atakayeshiriki katika kuwasaidia wahamiaji haramu kukatisha au kuingia nchini na kuwataka wananchi kuendelea kulinda amani iliyopo kwa kushirikiana vyema kufichua matukio ya kihalifu yanayotekea katika maeneo yao.




KATIKA MATUKIO MENGINEYO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma pia linawashikilia watuhumiwa Watatu wakazi wa Jiji la Dar es salaam kwa wizi wa Laptop pamoja na vitabu vyenye masomo mbalimbali yahusuyo ujenzi wa njia za treni na mambo mengine ya kitaamu ya Bwana Salehe Jabiri ambaye ni mfanyakazi katika Ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) ,tukio hilo limetokea tarehe 10,February 2022 katika Hoteli ya Holday iliyopo Makole Jijini Dodoma.

Katika tukio la tatu pia Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma Onesmo Lyanga amasema kuwa wanashikilia gari aina ya Isuzu yanye namba za usajili T 788- ASG iliyokutwa na mifuko 90 ya sementi zilizoibiwa mji wa Kiserikali wa Mtumba jijini Dodoma na tayari sementi hizo zimepelekwe mahakamani na kurudishwa Mtumba kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huku gari likiwa bado limeshikiliwa Polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.

Katika tukio la nne ni pamoja na Wizi wa Ipad 1,Laptop 1,Frigi 1 na pikipiki 1 hivyo Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma linawataka wananchi kama kuna aliyeibiwa moja kati vitu vilivyotajwa hapo juu afike kwa ajili ya kuvitambua.



Gari hili pia lipo chini ya uangalizi wa polisi mara baada ya kukamatwa likiwa na Sementi mifuko 90 iliyoibiwa katika mji wa Kiserikali wa Mtumba jijini Dodoma

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma Onesmo Lyanga akionesha Frigi lililopatikana na Askari baada ya kuibiwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga akionesha Screen nayo iliyopatikana na polisi baada ya kuibiwa

No comments:

Post a Comment