WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI KUJIIMARISHA ZAIDI MFUMO WA MTANDAO WA KIDIJITALI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 17, 2022

WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI KUJIIMARISHA ZAIDI MFUMO WA MTANDAO WA KIDIJITALI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA.



Na,Okuly Julius, Dodoma 
Katika kuhakikisha huduma za masuala ya ardhi zinatolewa kwa ufanisi Zaidi kwa wananchi,Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga kutoa huduma   za ardhi kupitia mfumo wa  mtandao wa kidijitali ambapo Zaidi ya Tsh.Bilioni 50 zilishatengwa kwa ajili ya  utekelezaji wa mpango huo.
Hayo yamebainishwa leo Februari ,17,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelina Mabula wakati akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Ofisi  za Wizara hiyo zilizopo Mtumba baina ya aliyekuwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.

Dkt.Mabula amesema Mtandao wa kielektroniki ni muhimu sana katika ufanisi wa utendaji kazi huku akibainisha kuwa Wizara yake itahakikisha wawekezaji hawakwami .

Aidha,Dkt.Mabula amezungumzia kuhusiana na suala la ukusanyaji wa kodi ambapo amesema kuna ulevi kwa baadhi ya wananchi wameujenga kuwa Mhe.Rais amezuia kodi hivyo wizara yake imejipanga ukusanyaji wa kodi ya ardhi unashika kasi.

Katika hatua nyingine ,Waziri huyo wa ardhi ametumia fursa hiyo kumpongeza Mhe.Lukuvi kwa kumjegea Uwezo pamoja na Rais awamu  wa awamu ya tano na awamu ya Sita kwa kumwamini.

Kwa upande wake waziri wa Ardhi ,Mstaafu William Lukuvi amezungumzia mafanikio ya wizara hiyo ikiwemo kuongeza ofisi za mikoa kutoka 6 hadi 26 huku akisisitiza ushirikiano  kwa watumishi wa wizara hiyo.

Ikumbukwe kuwa Mhe.Lukuvi amekuwa Waziri kupitia Wizara mbalimbali tangu mwaka 1995 na ndani ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametumikia kipindi cha miaka 8 ambapo Dkt.Mabula amesema ofisi yake itaendelea kumtumia kama  mshauri kwa changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza.


No comments:

Post a Comment