MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA MAKABIDHIANO YA JEDWALI LA UCHAMBUZI WA SHERIA NDOGO ZILIZOWASILISHWA KATIKA MKUTANO WA SITA WA BUNGE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 19, 2022

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA MAKABIDHIANO YA JEDWALI LA UCHAMBUZI WA SHERIA NDOGO ZILIZOWASILISHWA KATIKA MKUTANO WA SITA WA BUNGE.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akikabidhiwa taarifa ya Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Sita wa Bunge na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Kilumbe Ng’enda baada ya kikao kilichofanyika katika UKumbi wa Bunge Machi 18, 2022 Jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Kilumbe Ng’enda akiwasilisha taarifa ya Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Sita wa Bunge katika kikao hicho.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Bunge na Siasa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Ally Mfikirwa akieleza jambo katika kilichofanyika katika Ukumbi wa Bunge Machi 18, 2022 Jijini Dodoma.
Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Bwa. Mkuta Masoli akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika UKumbi wa Bunge Machi 18, 2022 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika katika UKumbi wa Bunge Machi 18, 2022 Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment