Na,Okuly Julius, Dodoma
MASHIRIKA 25 yameendelea na Kampeni ya Linda Ardhi ya Mwanamke ili kuondoa changamoto zilizopo katika umiliki wa ardhi ikiwemo mfumo dume.
Baadhi ya Mashirika hayo ni Shirika la wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF),Kituo cha Msaada wa Sheria kwa wanawake,chama cha wanasheria wanawake na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma March,17 mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa 66 wa pembeni wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani kwa njia ya mtandao,Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Umiliki wa Ardhi ( LANDESA),Nchini Dkt. Monica Mhoja amesema sheria za ardhi zilizopo nyingi ni nzuri tatizo ni kwenye utekelezaji wake.
Pamoja na hayo amesema kuwa imefika wakati mashirika mengeni ya serikali na yasiyo ya kiserikali kushirikiana na serikali katika nyanja mbalimbali hasa maeneo ambayo inaonekana haki za wanawake bado zinakandamizwa na kuhakikishi kwa Sheria zilizopo zisibaki kwenye makaratasi zifanye kazi kwa vitendo kwa maana ya utekelezaji.
Ameongeza kuwa LANDESA itaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa jamii ya kitanzania inatambua umuhimu wa kumiliki na kutumia ardhi kwa kufuata sheria na taratibu bila kuvunja katiba ya nchi,ikiwepo pia kuendana na kasi ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jukwaa la vyanzo asilia Tanzania TNRF Zakaria Faustine amesema katika suala la ardhi kuna changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo kwa kutumia teknolojia mbalimbali wanajaribu kuondoa changamoto hiyo.
Naye Mkurugenzi wa TAWLA Nchini Tike Mwambipile ameleza nafasi ya TAWLA katika kuhakikisha wanawake wanajua haki yao ya kumiliki ardhi,amesema kuwa wao wanajikiti katika kumtazama mwanamke,kufutilia sera,kutoa elimu na kuhakikisha kuwa wanawake wanapataiwa haki zaoza msingi katika jamii na taifa kwa ujumla ikiwemo katika kumiliki na kutumia Ardhi.
Amesema kuwa Mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo serikali,Landesa Tanzania na Oxfam utakuwa na tija kubwa kwa jamii kwa sababu umetumika kama jukwaa la kupaza sauti kwa jamii ili iweze kutambua nafasi ya mwanamke katika kumiliki ardhi.




No comments:
Post a Comment