| Mkurugenzi mkuu wa Shirika la LANDESA Tanzania Dkt.Monica Magoke Mhoja (Katikati) na Bi.Khadija Mrisho (wa kwanza kulia) |
Na Okuly Julius,Dodoma
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la LANDESA Tanzania Dkt.Monica Magoke Mhoja ,Amesema kuwa Shirika hilo limejikita katika kuangalia haki za masuala ya ardhi,usalama wa Ardhi kwa wananchi hasa kwa wale wanaoishi vijijini.
Amesema pia Shirika la LANDESA ni la kimataifa ambalo limeanzishwa mwaka 1981 na kwa hapa Tanzania limesajiliwa chini ya sheria za Asasi zisizo za Kiserikali katika kutete haki za Ardhi na matumizi yake.
Ameongeza kuwa kutokana na mkutano wa 66 wa Kamisheni ya hali ya watu uliofunguliwa march 14 na utafikia mwisho march 25 huu ,hivyo wao Kama Shirika la LANDESA wameamua kwenda sambamba na mkutano huo ndio maana wakafanya mkutano mtandaoni kutoa nafasi kwa wadau kujadili na kujifunza zaidi juu ya Haki za Ardhi kwa mwanamke hususani katika umiliki wa Ardhi.
Pamoja na hayo Shirika la LANDESA linaendelea kufuatilia matukio mbalimbali yahusuyo haki za Ardhi na matumizi yake hasa kwa makundi mbalimbali wakiwepo vijana ,Wanawake na Watu wenye ulemavu wanahusishwa kwa namna gani katika kutoa maamuzi ya kumiliki na kutumia Ardhi kwa haki na usawa.
Katika hatua nyingine amewataka wanawake wote nchini kutojidharau na kujiona wanyonge katika kushiriki shughuli mbalimbali katika jamii inayowazunguka na hali hiyo itawapelekea kujiamini na kushiriki katika ngazi mbalimbali ya maamuzi katika ngazi zote hasa masuala ya haki ya kumili ardhi.
Pia Dkt.Monica ameiasa jamii kuachana na mila kandamizi ambazo zimekuwa zikiwapa nguvu kubwa watoto wa kiume katika ngazi ya familia jambo ambalo linamfanya mwanaume awe na maamuzi ya moja kwa moja kwenye haki ya umiliki wa Ardhi kuliko mwanamke na hii kulingana na haki za umiliki wa Ardhi ni makosa.
Kwa upande wa wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Bi.Rennie Gondwe kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum amesema kuwa kwa sasa serikali imeweka maafisa Maendeleo ya Jamii kila ngazi kwanzia Taifa mpaka Mtaa jambo ambalo limesaidia sana wananchi hasa wanawake kupata haki zao kwa haraka bila kusumbuliwa.
Hivyo ,ameongeza kuwa kwa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa Mwanamke anahusishwa na kusimamia moja kwa moja katika ngazi zote za maamuzi hapa nchini.

No comments:
Post a Comment