VIDEO:HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA BENJAMINI MKAPA YAPATA ITHIBATI YA UBORA WA VIPIMO VYA MAABARA SASA VIPIMO VYAO KUTAMBULIKA KIMATAIFA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 21, 2022

VIDEO:HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA BENJAMINI MKAPA YAPATA ITHIBATI YA UBORA WA VIPIMO VYA MAABARA SASA VIPIMO VYAO KUTAMBULIKA KIMATAIFA.


Ithibati waliotunukiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa kwa kuwa ha vipimo bora vya Maabara.
Katika ya pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika akiwa ameshikilia ithibati hiyo


Na Okuly Julius, Dodoma

Msemaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jeremiah Mbwambo amesema BMH imepata ithibati ya ubora wa maabara na inafungua fursa ya utalii wa kimatibabu kwani yoyote anaweza kupima kwa kuwa vipimo vya maabara ya BMH vimepata ithibati hiyo.

Mbwambo ameyasema hayo wakati wakikabidhiwa Ithibati hiyo march 21,2022 na kuwapongeza watumishi wa maabara kwa kuhakikisha wanapata ithibati hiyo ya ubora kwa kuwa kuipata kunavigezo vingi, watumishi wa maabara wameonesha njia ya kushirikiana katika kazi na kufikia ubora wa juu.

Naye Meneja Maabara Hospitali ya Benjamin Mkapa Ndugu, Reuben Mkala amesema wamejipanga kuilinda ithibati hiyo kwa kufanya kazi zenye ubora, kuondoa malalamiko kwa wateja na kuhakikisha wanatoa huduma kwa wakati uliokusudiwa

Ameongeza kuwa, mafunzo ya kimaabara waliyopokea na nyaraka walizokuwa wakiandaa mara kwa mara, yalisaidia wakaguzi mbalimbali waliofika kukuta hatua za juu za ubora na hivyo ikawa ni kazi rahisi kupewa ithibati.

“Ndiyo maana katika maabara 37 tulizoomba ithibati wakati ule ya kwetu ikiwa changa kabisa kulinganisha na wengine tulikuwa kati ya maabara mbili zilizopewa ithibati wengine wemepewa hivi majuzi” Alisema Mkala.

Akitoa taarifa ya utendaji wa Idara na ithibati hiyo, Ndugu Susu J. Susu, Mkuu wa Ubora Maabara amesema maboresho ya huduma yalitokea kwa sababu ya kujiwekea malengo na namna ya kutathimini ufikiwaji wa malengo hayo.

“Tuliweka malengo mengi likiwemo la kupunguza malalamiko tunayopata katika Idara, vile vile kuhakikisha tunatoa majibu kwa wakati na kwa usahihi” Amesema Susu

Kwa mujibu wa Susu, Safari ya kupata Cheti cha Ithibati na kutambulika kimataifa kuwa miongoni mwa maabara yenye viwango vinavyokubalika haikuwa rahisi, iliwalazimu kuandika zaidi ya nyaraka 400, na kupokea mafunzo mbalimbali ya kusimamia na kuimarisha ubora wa viwango vya huduma za kimaabara ili kukidhi vigezo.

“Wakati mwingine tulilazimika kulala tukichakata nyaraka, na tulifanya mafunzo ya mara kwa mara kutoka wizarani na kwenye maabara nyingine, tunashukuru uongozi ambao uliendelea kutuunga mkono” Ameeleza Susu.

Kuwa na ithibati ya viwango vya ubora inamaanisha sampuli za uchunguzi zinazochukuliwa na kufanyiwa utafiti wa kimaabara zinaweza kutumika katika hospitali yoyote na kurahisisha mgonjwa kuhudumiwa.

Kwa maana hiyo pia humpunguzia gharama mgonjwa za kurejea vipimo kwa mara ya pili bila sababu za msingi na kurahisishia Madaktari wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kugundua matatizo halisi yanayowakabili wagonjwa na hivyo kutoa huduma za tiba kwa usahihi.


No comments:

Post a Comment