MAFURU ASEMA UBORESHAJI WA SOKO LA SABASABA JIJINI DODOMA NI KWA MASLAHI YA WAFANYABISHARA WENYEWE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 20, 2022

MAFURU ASEMA UBORESHAJI WA SOKO LA SABASABA JIJINI DODOMA NI KWA MASLAHI YA WAFANYABISHARA WENYEWE


MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru


Na Okuly Julius Dodoma

MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru amendelea kuwataka wafanyabishara wa soko la matunda na Mbogamboga Sabasaba kupisha ukarabati wa soko hilo huku akieleza lengo la serikali ni jema kwa maslahi ya wafanyabaishara hao na siyo vinginevyo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Aprili 20, 2022 Ofisini kwake amesema lengo la Jiji ni kuwahamisha kwa muda wafanyabiashara hao ili kufanya ukarabati wa soko hilo na baada ya ujenzi huo kukamilika watawarudisha kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

"Zoezi hili tunalifanya kwa uwazi,tuliwashirikisha wafanyabiashara wote na kilichobaki sasa ni kuhakiki ili kuwatambua nani anamiliki nini na anafanya nini na kuwaondoa hofu kuwa tunakwenda kuwahamisha kwa muda ili kupisha ujenzi wa eneo hilo kwa muda wa mwaka mmoja au miwili kulingana na mchoro wetu”amesema Mafuru

Aidha amesema soko hilo ni la historia na limechakaa kutokana na kuwa ni la muda mrefu tangu mwaka 1996 halijafanyiwa ukarabati wa miundominu yake hivyo ni wakati muafaka wa kuhakikisha linakarabatiwa kisasa zaidi kulingana na mahitaji na kuweza kuhudumia zaidi ya wafanyabiashara 7000 .

"Lengo la jiji ni kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na si kuwadhulumu,imefika wakati wafanyabiashara kuelewa Dodoma Sasa ni Jiji na ndiyo Makao makuu ya nchi na soko la Sabasaba limekuwa halina hadhi lazima tufanye ukarabati,"amefafanua na kuongeza;amesema Mafuru

Na kuongeza Kusema "Maana ikinyesha Mvua tope linakuwa la kutisha na nimekuwa nikipokea tunapokea simu za malalamiko kuwa tunachukua ushuru lakini hatufanyi ukarabati”amesema Mafuru

Amesema jiji halina lengo la kuwaonea wafanyabiasahara bali kinachotakiwa ni kuwashirikisha kila hatua ili kuweza kupata uelewa wa pamoja na kila mtu kuridhika na maamuzi hayo.

Hata hivyo amesema malalamiko ambayo wamekuwa wakiyapata yanaonyesha kuwa wafanyabiashara hao hawana imani na jiji katika kutekeleza mpango huo.

Amesema ili kupata kauli moja wanapanga kuendelea na vikao vya kujadilina baina ya jiji na uongozo wa soko hilo ili kupata namna bora ya kufikia mwafaka.

“Kuna watu wanahofu kupoteza vibanda vyao hasa wale wenye maeneo zaidi ya moja lakini ni wahakikishie kuwa kupitia mazungumzo tutafikia mwafaka na hakuna atakaye poteza haki yake waelewe tuu tunafanya uhakiki ili kujilidhisha na idadi ya wafanyabiasahara iliyopo”amesema

Kwa Upande wake Afisa Biashara ya Jiji la Dodoma Domitila Vedasto amesema soko la sababsa lina historia ya muda mrefu tangu mwaka 1996 waliahamishwa kutoka Nyerere Square na kupelekwa maeneo mbalimbali.

Pia amesema Soko la sababasa miundombini yake imechakaa na hata ukienda sasa hivi kuko wazi lakini pia hili ni jiji na makao makuu hatuwezi kuwa na soko la aina ile kama jiji tukasema kuwe na kitu cha kufanya kuboresha soko kama hadhi ya jiji na kuendana na makao makuu ya nchi.

"Tukawaza kuweka mkakati kwa maana katika mradi huu tutanza ujenzi mwezi wa saba na huwezi kuanza bila kuwashirikisha wadau ,vikao vimeanza tangu mwaka jana kuhusiana na changamoto kikubwa miundombinu vikao vya kuanza kujenza tumeanza mwezi wa kwanza wtaalam walikuja tukawashirikisha," amesema Afisa Biashara .

Na kuongeza Kusema "Siyo kwamba hatuja washirikisha wafanyabiashara tumewashirikisha . hii ni picha kwamba tunawashirikisha jambo wana mambo yao wanaona kama vile tunawaona lakini kimsingi tunawasirikisha,'' amesema

Naye Mkuu wa idara ya Fedha Jiji la Dodoma Rahabu Philip, alisema siyo kweli kuwa wafanyabiashara hao hawajashirikishwa katika mpango huo wa jiji.

“Tumekuwa tukiwashirikisha wafanyabiashara toka mwaka jana na ujenzi huu unatarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu baada ya serikali kutupatia fedha za kufanikisha ujenzi huu”amesema

Mwishoni mwa wiki iliyipita viongozi wa soko hilo wakizungumza na waandishi wa habari walidai kuwa wanapanga kufanya maandamano hadi Bungeni ili kufikisha kilio chao kwa waziri mkuu.



No comments:

Post a Comment