MAFUNZO ENDELEVU YA WATAALAM(CPD)YA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI YATUMIKE KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WAKE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, April 1, 2022

MAFUNZO ENDELEVU YA WATAALAM(CPD)YA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI YATUMIKE KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WAKE


Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Richard Mkumbo wa kwanza (kulia) wakati wa Mafunzo Endelevu ya Wataalam (CPD) ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) yanayoendelea jijini Dodoma. 



Na Okuly Julius Dodoma

Mafunzo Endelevu ya Wataalam(CPD) ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi)  Kuwajengea Uwezo Wataalam wake ili kuwa na uwezo wa kushiriki kwenye Miradi mikubwa.

Katika Mafunzo hayo Wataalam watapata fursa ya Kunolewa na Kubadilishana uzoefu katika mambo yanayohusu Taaluma za Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ili kuboresha uwezo wa Kitaalam kuendana na Mabadiliko ya Sheria, Kanuni,Sayansi na Teknolojia inayokuwa kwa Kasi kubwa katika Sekta ya Ujenzi na hatimaye kuongeza Tija na Ufanisi katika ukuaji wa Uchumi na Utekelezaji wa kazi zao za Kitaaluma.

Akifungua mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku mbili March 31,2022 na April 1,2022  Jijini Dodoma kwa niaba ya katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Richard Mkumbo amesema kuwa Mada inayohusu Masuala yanayojitokeza katika Sheria ya Kodi katika Sekta ya Ujenzi (Emerging Issues in Taxation Law in the Construction Industry in Tanzania) ni muhimu katika Taaluma za Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi kwa maendeleo ya Sekta ya Ujenzi na maendeleo ya Nchi kwa ujumla.

"Kuna umuhimu mkubwa wa kuimarisha ulipaji wa Kodi miongoni mwa Wadau na Wataalam wetu katika Sekta ya Ujenzi ili Shughuli za Ujenzi ziendelee kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na kupunguza kutegemea zaidi Wafadhili kutoka Nchi za Nje,"Amesema Mkumbo

Mkumbo amewakumbusha kuwa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) zilipata fursa ya kupeleka Watumishi wake kwenye Miradi Mikubwa ikiwemo ya ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Ujenzi wa Barabara na Madaraja pamoja na Ujenzi wa Kituo cha Kufua Umeme kwa lengo la kukuza ujuzi.

Akiongeza kuwa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ni mojawapo ya Taasisi zilizonufaika na Mpango huu wa Wizara hivyo watumie ujuzi huo kuhakikisha wanafanya kazi kwa ubunifu mkubwa ili kuleta tija katika sekta hii ya ujenzi.

Pia amegusia Mada ya “Mambo Muhimu ya Sheria ya Bodi Namba 4 ya Mwaka 2010 na Kanuni kuhusu Utozaji wa Ada za Ushauri kwa Kazi za Taaluma" (Salient Features of AQRB Act. No. 4 of 2010 and its Regulations Regarding Professional Fees and Related Remunerations on Professional Activities) inawakumbusha wajibu mkubwa wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuisaidia Serikali katika suala la udhibiti hasa wa Tozo na Makusanyo ya Ada za Ushauri na Usimamizi ili kukuza Nidhamu na Miendendo ya Wataalam wanaosimamia Miradi ya ujenzi ya Serikali au Waendelezaji Binafsi.

"Nimesikia kuwa kuna Mada nyingine kuhusu "Malipo ya Kodi kwa njia ya Kielektroniki na Kujaza Fomu za Ushuru”(Electronic Tax Return and Filling) ambayo itawasilishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)," Amehoji

"Bila shaka lengo la mada hii ni kuangalia namna bora ambayo inaweza kurahisisha Mawasiliano ya Wataalam na Mamlaka ya Mapato Tanzania.Katika suala la kuvutia Uwekezaji na Kudhibiti Kodi za Serikali katika Sekta ya Ujenzi kunahitajika Maboresho makubwa ya Kodi katika Sekta ya Ujenzi kama vile Kuchunguza uwezekano wa misamaha ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye vifaa vya ujenzi," Amesema Mkumbo

Maboresho ya Kodi yatasaidia na kusababisha kutoa mahitaji ya Walaji na Kujenga Ajira katika Sekta ya Ujenzi na Kuleta kazi na pesa nyumbani badala ya kwenda nje ni vema kufahamu kuwa miradi ya ujenzi ndiyo miradi inayotumia fedha nyingi kuliko miradi mingine hapa Nchini.

Shughuli za ujenzi zimeendelea kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi (asilimia 27.5), zikifuatiwa na kilimo (asilimia 25.8),usafiri na uhifadhi (asilimia 13.6) na shughuli za uzalishaji viwandani (asilimia 7.8)(chanzo ni Taarifa ya Ukuaji wa, 2020).

"Hivyo kutokana na taarifa nawasihi Wataalam wote kuzingatia Sheria na Kanuni za Kodi wakati wa utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi liwe jambo linalopewa kipaumbele,"Aliongeza Mkumbo

Bodi zenye Mamlaka ya Usimamizi katika Sekta ya Ujenzi zikiwamo AQRB,ERB,CRB,NCC, na Mamlaka nyingine zina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa Wataalam wanaopewa dhamana ya kutekeleza miradi ya Ujenzi wanazingatia Sheria za Kodi katika utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi.

Ameongeza pia Katika baadhi ya Miradi ya Ujenzi inayosimamiwa na kutekelezwa na Wataalam wa Ndani, ukwepaji wa Kodi umekuwa mkubwa kiasi cha kusababisha Malalamiko dhidi ya Umahiri na Ujuzi wa Kampuni zetu za Ndani,Kaguzi ambazo zimekuwa zikifanywa na Mamlaka za Usimamizi kwenye miradi ya Ujenzi, zimebaini mapungufu makubwa katika ubora wa kazi na gharama za Miradi.

"Wakadiriaji Majenzi kwa usikivu mkubwa niwaombe mjadili kwa Umakini Mada zitakazowasilishwa mbele yenu leo na kesho katika Mafunzo haya ili hatimaye mtoke hapa mkiwa na uelewa mpana zaidi katika Taaluma yenu hii muhimu ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,"Amesema Mkumbo

"Nitapenda kupatiwa Maazimio ya Mafunzo Endelevu ya Wataalam ili Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi iyafanyie kazi," Amemalizia

No comments:

Post a Comment