MTOTO ALIYEUWAWA NA KUTUMBUKIZWA KWENYE PIPA, WAZIRI GWAJIMA AFIKA ATOA SALAMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 16, 2022

MTOTO ALIYEUWAWA NA KUTUMBUKIZWA KWENYE PIPA, WAZIRI GWAJIMA AFIKA ATOA SALAMU


Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akiongea na Mama wa Mtoto Mage aliyeuwawa kikatili na anayedaiwa Kuwaita ni Mama yake Mkubwa Nyumbani kwa Mama huyo eneo Mabibo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Peter Nsanya, akiongea wakati Waziri alipofika kutoa Pole kwa Familiya ya Mama Mage eneo la Mabibo kufuatia kifo cha Mtoto huyo kilichotokea kikatili wa Mama Mkubwa.
Baadhi ya Wananchi wa Eneo la Ubungo wakiwa wamekusanyika wakati wa Ziara ya Waziri Gwajima katika eneo hilo na kutoa Pole kwa Wafiwa
Shaidi aliyefahamika kwa Jina Furaha Pius akimsimuliwa Waziri Gwajima jinsi alivyo mfahamu Mtoto huyo kabla yakukutwa na mauti.

Na WMJJWM-Dar es Salaam.

Waziri wa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amezitaka Mamlaka za Serikali za mitaa na Kata zihakikishe zinafuata mwongozo wa uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ili kupunguza matukio ya ukatili kwa watoto nchini.

Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Aprili 16, 2022 alipotembelea familia ya mtoto  miaka miwili na miezi minne, aliyefahamika kwa Jina la Mage,  aliyedaiwa kuuawa kikatili na mama yake mkubwa aitwaye Latifa Bakari (33) mkazi wa Mabibo mkoanj Dar es salaam.

Dkt. Gwajima amesema Kamati za ulinzi wa Mwanamke na Mtoto kwenye mtaa zijipange kujua na kufumbua maovu yanayotendeka katika jamii kwani vitendo vya ukatili vingi vinatokea katika ngazi ya familia na havigunduluwi maana vinamalizwa kimya kimya.

"Inasikitisha huyu mtoto alikuwa anaonyesha wazi namna ambavyo hana amani hapa anapoishi, lakini Mjumbe wa Shina aliambiwa hakulichukulia hatua mpaka mtoto ameuawa, naagiza nchi nzima ngazi za Serikali za mitaa na Kata anzisheni klabu za kukutana na watoto watasema wanayoyapitia,” alisisitiza Dkt. Gwajima

Aidha Waziri Dkt. Gwajima ametoa rai kwa jamii kuhakikisha wanatoa taarifa kabla ya kuchukua hatua na kwa wazazi ambao wameshindwa malezi ya watoto watoe taarifa kwa maafisa Ustawi wa Jamii kuliko kuua, kutelekeza au kupiga kupita kiasi watoto.

“Tunao watoto wanaokimbilia mitaani, kabla hujabariki hilo tunaomba uchukue jukumu lako kukumbuka kwamba Rais ameiunda Wizara hii na wapo maafisa wa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kwenye Kata mnachotakiwa kufanya mpelekee huko waambie wao wanaweza kufanya upembuzi yakinifu wa tatizo lako.” alisema Dkt. Gwajima

Hata hvyo Waziri Dkt. Gwajima amesisitiza kuwa anataka kuona slSheria ikichukua mkondo wake na mtuhumiwa akifikishwa mahakamani ili haki itendeke.

“Mlishindwa kujadili kindugu wakati mtoto anateswa kwa sasa Wizara tutaifuatilia hatutaki kuona watu wanafanya ukatili kwa wanawake na watoto mpaka wanafikia hatua ya kuua kabisa, halafu mnataka kukaa kifamilia tutawatetea watoto kwa ustawi wao, wazee na wanawake.” alisema Waziri Gwajima.

Akimsimilia kisa hicho, Mkazi wa Mabibo Kisimani, Furaha Pius amesema mtoto alikuwa na alama nyingi za vipigo na nilishawahi kumwambia Mjumbe wa Shina kuhusu suala hilo ili aweze kuchukua hatua au kutoa taarifa sehemu husika dhidi ya kitendo hicho.
 
Kwa Upande wake Mama Mkubwa wa mtoto huyo, Mariam Damas alisema majirani wamesema kwamba mtoto huyo alikuwa akipigwa kila siku kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukojoa kitandani lakini sio sahihi kumpiga mtoto huyo kwa kiasi hicho cha kinyama vitendo hivi lazima vikomeshwe.

“Lakini suala la mama yake kumleta mtoto huku sisi hatukuliafiki na wakati tunataka kuchukua hatua haya yakatokea ” alisema Mariam

“Tunaiomba Serikali ichukue hatua kwa sababu mume wa mtuhumiwa anataka kumwekea dhamana mkewe atoke, sisi tunaomba tena sana haki itendeke maana wameshaanza kutaka limalizwe kifamilia.” alisisitiza Mariam

No comments:

Post a Comment