Na. Mwandishi wetu Dodoma
SADAKA yako inafweza kunena vyema mbele za Mungu Kama Kornelio ukisoma katika Biblia Matendo ya Mitume 10:1.2 toa kwa Imani maana Imani ni kuwa na Hakika ya Mambo yatarajiwayo,hivyo taraji kitu kutoka kwa Bwana.
Mchungaji wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT ) Ilazo jijini Dodoma Wisdom Gowele amewasihi Wakristo kuweka Imani zaidi katika kutoa uko ndiko kunafunguo za Baraka Amezungumza hayo jumapili iliyopita katika Ibada ya Neno la Mungu.
Mchungaji Gowele alitoa alishuhudia matendo makuu ya Mungu tangua alipoanza kutoa Alisema Mimi naamini kutoa nimwemwona Mungu akinisaidia katika nyakati tofauti nilizopitia, sijawahi kupungukiwa Bwana Yesu asifiwe, siku moja mtu aliniuliza hapa pango unalipa Bei gani? Nilipo mtajia alishangaa akasema pesa zote hizi unatoa wapi? Mtu mwingine akasema mbona unavaa Sana suti pesa za kununua nazipata wapi? Nikawajibu siku zote mtu anayetoa anaongezewa , nimemwona Mungu katika kutoa, nikitoa kitu kwa wahitaji napokea kitu, nikitoa suti napokea suti kutoka kwa wapenda Kuna siku nilikusanya pea kumi za viatu nikazigawa zote kesho yake nikapewa pea tatu za viatu vizuri Sana, nikitoa shati napata shati nikitoa pesa napata pesa mpigie Yesu makofi ya Sifa alisema.
Pia mchungaji Gowele aliwakumbusha waumini wake kuwa Alisema siku zote ukitoa sifuri tambua ya kwamba na wewe utapokea sifuri, imeandikwa jinsi mtu anavyotoa ndivyo atakavyopokea mithali 16:1.3 Usitoe kwa manunguniko au kwa kujisifia Alisema .
Kwa upandea wake Bishop. Magnus Swedy wa kanisa la EAGT Miyuji alitangaza Aliwabariki Bi.Jenipher Gowele na Bw.Jonson Kitemi kwa hatua yao nzuri ya kutangaza uchumba na kuheshimu sheria na kanuni za ukristo.
Alisema Uchumba sio ndoa kamili ni mausiono tu ya awali baina ya mwanamke na mwanaume,hivyo ninayo furaha kuwatangazia kuwa Jonson na Jenipher kwa Sasa ni wachumba tu bado hawajaingia kwenye ndoa hiki kitendo kitachotendeka leo ni makubaliano ya ya karibu yasiyo na husisha vitendo vya ndani ya Ndoa Alisema Bishop Magnus Swedy.




Amen Ubarikiwe
ReplyDeletekijana