Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.
Akimzungumzia mtangulizi wake huyo, Rais Uhuru Kenyatta amemsifu kwa kusema alikuwa kama baba katika historia ya Kenya.Taarifa ya kifo chake imetangazwa leo na rais Uhuru Kenyatta aliyemtaja kama kiongozi aliyesifika nchini humo.
Siku kadhaa za maombolezo zimetangazwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambazo zitaendelea hadi yatakapofanyika maziko. Aidha Rais Kenyatta amesema Kibaki ameiacha Kenya ambayo ina mshikamano zaidi na maendeleo.
Alikuwa rais wa tatu wa Kenya tangu ilipojipatia uhuru kutoka Uingereza mwaka 1963 na aliingia madarakani kuanzia mwaka 2002 hadi 2013. Wakenya wengi walimtazama kama mwanasiasa na mtu aliyeleta mageuzi ya kiuchumi nchini humo.
Kuingia kwake madarakani kuliufikisha mwisho utawala wa chama kimoja cha KANU nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment