Na Okuly Julius Dodoma
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Teknolojia na Sayansi ya Nyuklia yenye lengo la kujadili na kupitia Rasimu ya mpango wa maenedeleo wa miaka mitano kwa ushirikiano na Tume ya nguvu za Atomiki Dunia ,kaimu katibu mkuu wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Maulilo Kipanyula amesema kuwa tume ya nguvu za Atomiki Tanzania imekuwa na msaada mkubwa sana kwa taifa katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya,maji pamoja na Kilimo na Ufugaji.
Prof.Maulilo amesema kuwa mpango wa maendeleo ya miaka mitano wa Tume ya nguvu za atomiki Tanzania ni vyema ukavipa vipaumbele masuala yaliopo kwenye Dira ya mpango wa taifa ili kuendelea kuletea taifa mafanikio makubwa hasa katika matumizi salama ya Nyuklia.
"Kama nchi tunanufaika sana na uwepo wa tume hii hivyo ushauri kwenu ni kuhakikisha mnafanya kazi kulingana na Dira ya maendeleo ya Taifa hapo mtakuwa mmeyagusa maisha ya watu wa chini kabisa ila nisiache kuwashukuru Tume ya nguvu za Atomiki duniani kwa kuendelea kuwezesha vifaa pamoja na pesa ambazo zimekuwa zinatusaidia katika sekta mbalimbali hapa nchini kwetu," Amesema Prof.Maulilo
Pia Ameipongeza tume hiyo kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kusaidia upatikanaji wa mashine za Mionzi kwa ajili ya wagonjwa wa Saratani nchini yenye thamani ya Bilioni 33.4 pamoja na kuendelea kuwasomesha wataalamu wa mionzi.
Katika sekta ya Kilimo Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania imefanikiwa kuzalisha mbegu bora mfano mbegu bora ya Mpunga na kufanikiwa kujenga mpango wa kuzalisha Liquid Nitrogen huku Visiwani Zanzibar.
KWA upanda wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za atomiki Tanzania Prof.Lazaro Busagala amesema kuwa mkutano huo wa wadau wa Teknolojia na Sayansi ya Nyuklia utakuja na mpango wa miaka mitano baada ya kupitia rasimu iliyosheni vipaumbele zaidi ya sita kutoka kwenye sekta mbali mbali za maendeleo hapa nchini
Prof.Lazaro Busagala amezitaja vipaombele vilivyopo katika rasimu hiyo kuwa ni Afya,Chakula na Kilimo,nishati,rasilimali watu, Lishe,viwanda na Uendelezaji wa rasilimali watu hivyo ni rasimu ambayo itamgusa kila mtanzania.
" Malengo yetu kama Tume ya nguvu za atomiki Tanzania ni kuhakikisha kila mtanzania mwenye tatizo la saratani aweze kutibiwa na kupata huduma hiyo kwa urahisi," amesema Prof.Lazaro Busagala




No comments:
Post a Comment